Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa tatu kutoka
kulia), akiongea na fundi ambaye anafanya shughuli za ujenzi katika
Daraja la Reli la Bahi-Kintinku. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara
kwenye daraja hilo na kupata taaarifa kuwa limekamilika kwa asilimia
98. Aidha daraja hilo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (wa pili kutoka
mbele), akishuka chini ya daraja la bahi-kintinku kuangalia maendeleo ya
ujenzi wake. Daraja hilo linajengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC). Kukamilika kwa daraja hilo kutasababisha Treni za abiria na mizigo kupita kwa uhakika majira yote ya mwaka.Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi wa mradi kutoka kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation(CCECC),
Bw. Wang Chao(aliyevaa fulana ya rangi ya karoti), wakati alipotembelea
mradi huo mapema wiki hii. Ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa
asilimia 98 na litakabidhiwa kwa Serikali mapema tarehe 28 Novemba 2013.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment