Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji (kushoto), Afisa Habari – Baraka Kizuguto na Beno Njovu Katibu Mkuu mpya(kulia)
Mwenyekiti
wa Young Africans Yusuf Manji leo amemtambulisha rasmi Bw. Beno Njovu
kuwa katibu mkuu mpya wa klabu akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako
aliyekua kaimu katibu mkuu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Mwenyekiti wa
Yanga Bw.Yusuf Manji amesema Beno Njovu anaanza kuitumikia hiyo nafasi
mpya kuanzia leo na Mwalusako atakua nae pamoja kwa kipindi cha mwezi
mmoja mpaka atakapokabidhi kazi rasmi.
Aidha
Manji ametangaza mkutano mkuu wa wanachama Januari 19,2013 ambapo
wanachama watapata fursa ya kupitia mapato na matumizi, na ajenda
zingine mbalimbali ambazo zitajadiliwa katika mkutano huo.
Kikao
cha kamati ya utendaji kilichoketi mwishoni mwa wiki kimemteua Bw.Seif
Ahmed “Magari” kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa na
kutokana na nafasi hiyo pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya
Utendaji wa klabu ya Yanga.
Katika
mkutano na wandishi wa habari makao makuu ya klabu Manji ametangaza
rasmi kutogombea tena uenyekiti katika uchanguzi mkuu ujao, hili
nimeliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa nimefuata
demokrasia.
Nina
miezi saba kabla ya uchanguzi mkuu mwakani hivyo sasa ninajitahid
kukamlisha shughuli zote ambazo nilianza kuzifanya ndani ya Yanga nikiwa
kama mwenyekiti ili uongozi mpya utakaoingia uweze kuendeleza mipango
ya kuifanya Yanga iwe klabu bora Tanzania.
CHANZO: DAR YOUNG AFRICANS OFFICIAL WEBSITE
No comments:
Post a Comment