WILAYA YA CHUNYA – AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 09.12.2013 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
NAMKUKWE, KATA YA NAMKUKWE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA, PIKIPIKI NO. T.221 CJD AINA YA FEKON IKIENDESHWA NA SIKUJUA S/O
JIMSON, MIAKA 25, MNYIHA NA MKAZI WA NAMKUKWE ILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU AITWAYE BIALES D/O MAJIYATAMU, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA
MIAKA 50-60, MNYIHA NA MKAZI WA NAMKUKWE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO
HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI HASA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA
MWISHO WA MWAKA 2013 ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA ABIRIA KUTOSHABIKIA MWENDO KASI KWANI UNAUA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 09.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO NONDE, KATA YA NONDE,
TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIWAKAMATA 1. FELIX S/O ODEN, MIAKA 19, MKULIMA NA MKAZI WA NONDE NA
2. MARKOS S/O GERALD, MIAKA 25, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA
WAKIWA NA BHANGI KETE 07 SAWA NA UZITO WA GRAM 35. WATUHUMIWA WOTE NI
WATUMIAJI NA WAUZAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZINAFANYWE ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA
ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment