Didier Drogba
Kitendo
cha Didier Drogba na Emmanuel Eboue kuvua jezi na kuonesha ujumbe wa
kumuenzi Mandela katika fulana zao kimewaingiza matatani.
Tukio hili lilitokea mchezo ulipoisha baada ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya timu ya SB Elagizspor.
Drogba
alivua jezi yake na kubaki na fulana iliyokuwa na maneno yaliyosomeka
"Asante Madiba; wakati Eboue katika fulana yake akimtukuza kwa ujumbe
wa "Pumnzika kwa Amani Nelson Mandela"”.
Hata
hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Kamati ya nidhamu ya Shirikisho
la Soka la Uturuki (TFF) lilitafsiri tofauti tukio hilo na kuwataka
Drogba na Eboue kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Wachezaji
hawa walifanya tukio hili baada ya mchezo kuisha lakini wanaweza
kufungiwa kwa kuwa TFF inakataza wachezaji kuonesha ujumbe wa kisiasa
mchezoni.
Chanzo: Au.Sports
No comments:
Post a Comment