Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 31, 2013

HIDAYA NJAIDI AJALI IMENIWEKA KILEMA NAFULIWA HADI NGUO ZA NDANI


Hidaya-Njaidi f.jpg cut 531Msanii mahiri katika tasnia ya Filamu Bongo Hidaya Njaidi yupo katika wakati mgumu kutokana na ajali aliyoipata kipindi cha nyuma ambayo imepelekea mkono wake wa kushoto kuvunjika na kushindwa kupona ukiambatana na maumivu makali. 
Hidaya-Njaidi f  
  njaidi p 531  


“Kabla hujafa hujaumbika mimi nilikuwa mtu wa kujituma katika shughuli zangu, lakini tangu nipate ajali nimekuwa si uwezo huo, kwa sababu nashindwa kufanya chochote yaani mkono wangu hauna nguvu ya kuinua hata kikombe cha chai, imefika hatua hata nguo zangu za ndani nasaidiwa kufuliwa na familia yangu, hata kuigiza naigiza nafasi chache ambazo ni za kawaida maana sitakiwi kutumia nguvu , nimehangaika Hospitali kadha za hapa Bongo lakini imeshindikana ushauri niliyopewa na Madaktari nikatibiwe nje ya nchi,”alisema Hidaya.

Akizungumza na paparazi Msanii huyo akiwa nyumbani kwake alisema kuwa ajali aliyoipata kipindi cha nyuma imemrudisha sana nyuma katika kazi zake na kutafuta maendeleo katika familia yake, ajali hiyo inamfanya ashindwe kuwa hata na furaha kwenye jamii inayomzunguka.

No comments:

Post a Comment