Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 31, 2013

MAUWAJI YA KINYAMA IRINGA MWANAMKE AUWAWA KWA KUCHOMWA VISU MMOJA AJERUHIWA VIBAYA

Waombolezaji  wakiwa  katika msiba  huo  eneo la Mtwivila 
Mume wa marehemu Bw Hamza Kidava na mtoto wake  wakitoa heshima  za mwisho  kabla ya mazishi 
mwili  wa marehemu Doris Lyandala
Kaburi la marehemu Doris
Aliyekuwa  mume wa marehemu Doris Lyandala Bw Hamza Kidava kushoto akiwa na rafiki  zake nyumbani kwao Mtwivila leo
Bw Hamza Kidava  akiwa katika majonzi mazito
Bw Hamza Kidava  akionyesha  eneo  ambalo mke  wake kipenzi alipouwawa kwa  kuchomwa visu na mtu anayesadikika kuwa ni kichaa
Bw Hamaza kushoto akimwonyesha mwandishi wa mtandao huu mzee wa matukio  daima hayupo pichani na Bw Brown eneo ambalo mke  wake aliuwawa
Dereva  Taxi  aliyekuwa akimwendesha  Mzee wa matukio  daima  Bw Brown akiwa nje ya nyumba aliyekuwa akiishi mtuhumiwa wa mauwaji  ya Bi Doris Lyandala
HAKUNA Kati  yetu  ajuaye siku yake na  kufa na kifo  chake kitakuwaje na kama ungelijua lijalo mbele  yako hakuna ambaye angejaribu kutoka ndani ya nyumba yake kwenda  kukutwa na mauti.
Ni kauli  za  majirani  na marafiki wa karibu wa mrembo Doris  Lyandala  ambae kwa sasa kwa wakazi wa mji wa Iringa jina lake  ndilo limeendelea kutesa mawazo ya  wengi.
Doris ambae enzi za uhai  wake alipata  kuwa mmiliki wa Saloon yake ya kutengeneza  nywele  warembo wenzake na alipata kuwa mcheshi asiyependa makuu tulitamani tungekula na  kusherekea nae pamoja  Krismas  ambapo ilibaki siku moja pekee kula Krismas na rafiki ,familia yake na  zilibaki  siku takribani  7  kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ila yote hayakuwezekana na badala  yake rafiki na ndugu walijikuta  katika simanzi ya kifo chake .
Mmoja kati ya marafiki zake wa karibu  Salima Alli alisema  kuwa alikuwa ni mteja  wake mkubwa katika  saloon na kabla ya  kukutwa na umauti  siku moja kabla alipata  kumseti nywele  zake.
Bw Hamaza Kidava  ndie mume wa marehemu  huyo anasema kuwa alipata  taarifa  kutoka kwa majirani  kuwa kipenzi chake mke wa mtoto mmoja amepatwa na tatizo na amekimbizwa katika  Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa baada ya  kufika Hospital hapo hakuamini  kuona mke aliyempenda kuliko akitokwa na damu huku akieleza kwa  shida  kilichomkuta .
Akizungumza kwa uchungu mwigi huku akilengwa na machozi Hamza ambae ni mmoja  kati ya vijana watanashati na wenye ajira zao akiwa katika  sekta ya kutengeneza simu alisema  kuwa alichoelezwa  kuwa amechomwa visu na kichaa.
"Ina  niuma  sana  kumpoteza mke  wangu na ina niuma sana kuona  leo  nimebaki mpweke nikilea mtoto mmoja ambae nimezaa nae mke  wangu Doris ....kaka nashukuru kwa  kuja  kunifariji na  nawashukuru wote  walioshiriki kuuguza hadi mazishi  yake "alisema Hamaza  kumaliza kwa kusema twende nikakuonyeshe alipokutwa na mkasa huo  wakati akitoka dukani kutafuta mahitaji.
Ndudu wa karibu na mtuhumiwa wa mauaji  hayo ambae hakupenda  jina lake  kuandikwa hapa kwa kuwa si msemaji wa familia alisema  kuwa  mtuhumiwa  huyo wa mauwaji Bw Zakayo Lwambano (26) ni mkazi wa Mtwivila na alikuwa akiishi  mtaa mmoja na marehemu Doris .
Alisema  kuwa kijana  huyo Zakayo alianza kuugua ugonjwa  huo toka mwaka 2010 ambapo ndugu  walimpeleka Hospital ya vichaa Milembe Dodoma na kurejea akiwa mzima wa afya.
Hata  hivyo alisema  baada ya  kurejea  alikuwa ni mtu aliyetulia na kujipatia  kipato chake cha kila siku kwa  kufanya kazi ndogo ndogo za kusomba mchanga na nyingine kwa  wananchi wa eneo hilo .
Ndugu  huyo alisema wazazi wa mtuhumiwa huyo kwa  sasa  walisha fariki dunia na alikuwa akiishi peke yake katika getho ( nyumba yake ya chumba kimoja )  aliyojenga  mwenyewe   
Alisema  kuwa  siku ya tukio Desemba 24 kabla ya kumshambulia Mrembo  huyo alianza kumchoma  kisu ndugu  yake James Moyo (28) ambae  alifika nyumbani hapo kwa  ajili ya kula sikukuu  akitokea Makambako Njombe.
Alisema kijana  huyo aliyejeruhiwa alikuwa akiishi nyumba nyingine tofauti na getho la mtuhumiwa na alichomwa  visu viwili kwapani na kukimbizwa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa na kwa sasa ameruhusiwa na kurejea Makambako kwao.
Pia  alisema mtuhumiwa  huyo baada ya mauwaji alijipeleka mwenyewe polisi na kutaka awekwe ndani kwa madai ameua
Jeshi  la  polisi  mkoa wa Iringa  limethibitisha  kutokea kwa mauwaji hayo na kuwa  mtuhumiwa huyo hadi sasa anashikiliwa na polisi .
Kamanda wa  polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa mwanamke  huyo alichomwa visu sehemu mbali mbali ya mwili  wake na baada ya  kukimbizwa  Hospital akiendelea na matibabu alifariki dunia.
Alisema kuwa   mtuhumiwa   huyo amenashikiliwa kama  watuhumiwa wengine na kuwa mwenye mamlaka ya kumfunga ama kutomfunga ni mahakama na  wao kama polisi hawajui kama ni kichaa wanajua kama mtuhumiwa wa mauwaji.
Mtandao  huu na  wadau wake  unatoa pore  nyingi kwa familia ya Kidava na Lyandala pamoja na ndugu na jamaa wote ambao  wameondokewa na mpendwa  wao ambae sote  tulimpenda  sana ila Mungu kampenda zaidi yetu  hivyo hatunabudi kusema jina lake  lihimidiwe milele yote


Chanzo;Fransis godwin blog

No comments:

Post a Comment