………………………………………………………………………..
Mwaka 2013 ukiwa unaelekea ukingoni, umekuwa wa huzuni kwenye tasnia ya filamu kutokana na wasanii wengi kupoteza maisha.
Pia katika mwaka huu wa 2013
kumetokea vifo vya wasanii na kuacha mapengo kwenye tasnia hiyo kama
ifuatavyo, Januari 2, mwigizaji Juma Kilowoko almaarufu Sajuki alifariki
dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kifo chake siyo tu kiliacha
pengo bali kilistua watu kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanyika
kuokoa maisha yake, ikiwemo kwenda nchini India kupata matibabu.
Lakini cha kufurahisha aliyekuwa
mkewe Wastara Sajuki anaendelea kufanya kile alichokuwa akifanya na
mpendwa mumewe yaani kuendeleza kuigiza, ni matumaini atayafanyia kazi
yale yote yaliyokuwa yakifanywa na marehemu mumewe.
Januari 8, msanii maarufu wa
miondoko ya muziki wa mnanda au mchiriku, Omari Omari alifariki dunia
baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuthibitika kuwa alikuwa anaumwa kifua
kikuu.
Omari Omari ni miongoni mwa vijana waliojipatia umaarufu kupitia muziki huo unaopendwa zaidi maeneo ya uswahilini.
Aprili 17, mwanamuziki mkongwe
katika miondoko ya taarabu na muziki wa mwambao Fatuma Binti Baraka
maarufu Bi Kidude alifariki dunia na kuzikwa visiwani Zanzibar, ambako
ndiyo nyumbani kwao.
Msiba wa Bi Kidude ulihudhuriwa
na waombelezaji wengi ikilinganishwa na msiba wa mwigizaji Steven
Kanumba, ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo
wanasiasa.
Mei 28, mwanamuziki mahiri wa
muziki wa Hip Hop Albert Mangwair maarufu Mangwea, alifariki dunia
nchini Afrika Kusini katika Hospitali ya St Heleni Joseph jijini
Johannesburg na kuzikwa nyumbani kwao Morogoro.
Mwanamuziki huyu, alipata maziko
ya kutukuka huko nyumbani kwao Morogoro baada ya kuwa na maandano
ambayo hayakuwahi kutokea , hata mapokezi ya mwili wake ulipofika Uwanja
wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere yalikuwa ya kihistoria, kutokana na
watu kufurika na kusukuma gari lililobeba mwili wake hadi maeneo ya
Tazara jijini Dar es Salaam.
Julai 13, mwanamuziki wa Hip Hop
Langa Kileo alifariki dunia, Julai 10, mwigizaji Kash maarufu Jaji
Khadija alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa
amelazwa, aliwahi kutamba na igizo la ‘tamu chungu’.
Septemba
8, mwigizaji Zuhura Maftaha, maarufu Melisa alifariki dunia, ingawa
wakati anafikwa na umauti alikuwa anafanya shughuli nyngine baada ya
kujitoa kwenye masuala ya uigizaji.
Novemba
11, mtangazaji wa kipindi cha taarabu cha Passion FM, na mwanamuziki wa
miondoko hiyo Nyawana ‘Matashtiti’ Fundikira, alifariki dunia, nyimbo
aliyowahi kutamba nayo ni ‘nipo kamili nimejipanga’.
Nyawana alizikwa nyumbani kwao Tabora ikiwa ni kutekeleza kauli yake aliyoitoa akiwa hai kuwa akifa akazikwe kwao.
Imeandaliwa na Kalunde Jamal
Kalunde Jamal
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment