Polisi wanasema kuwa bomu hilo lilitegwa kando ya barabara eneo la watembea kwa miguu na lililipuka mara tu basi hilo la abiria lilipokaribia eneo hilo
Idara za usalama zimeiambia BBC kuwa wataalamu wa milipuko wamegundua kuwa kulikuwa na bomu jingine lililokuwa limetengwa karibu na kwenye ubao wa matangazo hatua chache kutokea pale lilipolipuka la kwanza
Shambulizi hili la bomu limetokea huku siku ya jumanne wiki hii kukiwa na mlipuko mwingine wa bomu ndani ya gari katika jingo la walinzi kaskazini mwa mji wa Mansoura ambapo watu 16 walifariki dunia na wengine 100 kujeruhiwa
Serikali inalituhumu kundi la Muslim Brotherhood kuhusiaka na tukio hilo japo kuwa kundi hilo limekanusha madai hayo. Kundi la wapiganaji wa kiislam linalodaiwa kushirikiana na kundi la kigaidi la al qaeda la Ansar Beit al-Maqdis (Champions of Jerusalem) limekiri kuhusika na shambulio hilo.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment