MZEE huyu
wa jamii ya kabila la wamasai aliyetambulika kwa jina la ''Tulito''
Mkaazi wa KIAnjia panda ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kilimanjaro
International Airpot, Leo mda mfupi uliopita amepata ajali mbaya ya kugongwa
na fuso alipofanya jaribio la kuvuka barabara hio ya lami ambayo magari
huenda mwendo kasi, Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka mkoni
kilimanjaro
kimedai
kwamba gari hilo aina ya FUSO halikusimama baada ya kumgonja mzee Tulito
lilitokomea..! Raia waliokuwa karibu na eneo la tukio hawakufanikiwa
kunasa walau hata namba za gari hilo, Mzee tulito aliwahishwa Hospitali
wilayani boma kwa matibabu zaidi.
CHANZO : MATUKIO NA MICHAPO
No comments:
Post a Comment