Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 12, 2013

TAARIFA MUHIMU KUTOKA WIZARA YA MAWASILIANO KWENDA KWA WATUMIAJI WOTE WA SIMU,ISOME TAARIFA HIYO HAPA



Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame 

 Mbarawa Serkali imewaonya kuwa itawachukulia hatua watu wanaosajili namba za simu kwa kutumia majina kwa kuwafunga miezi sita jela au kutozwa faini.
Onyo hilo lilitolewa Bungeni na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, aliyetaka watu wenye tabia hiyo kwa lengo la kufanya uhalifu, kutuma ujumbe wa matusi na mengineyo watachukuliwa hatua gani.

Profesa Mbarawa alisema suala la usajili wa namba za simu ni la kisheria na linaendelea vizuri lakini kwa yeyote anayesajili simu kwa majina bandia, akibainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso, alitaka kujua sababu za kusuasua mipango ya kuweka minara ya mawasiliano katika kata za Katuma na Sibwesa.
Akijibu swali hilo, Waziri huyo, alizitaja kuwa ni mvuto mdogo wa kibiashara katika maeneo husika yanayotokana na hali za kijiografia kutokana na wingi wa milima na mabonde, misitu na kuwapo kwa idadi ndogo ya watu.

Alisema Serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote una lengo la kufikisha mawasiliano hususani katika maeneo ya vijijini kwa kuyaainisha maeneo yenye hali hii na kuyaweka katika mpango wa kufadhili upelekaji wa mawasiliano.

Alisema maeneo ya vijiji vya kata za Katuma na Sibwesa yapo katika zabuni ya awamu ya kwanza B kwa gharama ya fedha za ndani.
 TUNAOMBA CLICK IYO LINK NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI NA UPDATES TOFAUTI TOFAUTI

No comments:

Post a Comment