Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini (picahni)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya
wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 sawa na asilimia 96.15 waliofaulu
mtihani wa darasa la saba 2013 wataanza kidato cha kwanza mwaka ujao.
Kati
yao wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na huku kiwango cha
wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu wakiwa wameongezeka kwa asilimia
31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza
mwaka huu.
Matokeo
yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana 218,093 na
wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938
waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha
ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment