Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza. |
Meneja wa The Great Zone Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa matarajio ya Kampuni. |
Baadhi ya Maaskofu. |
Bahati Bukuku naye alikuwa sehemu ya waalikwa kwenye hafla hiyo. |
Sala ya kuhitimisha hafla. |
Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika hafla hiyo. |
MWANZA:Naibu
Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba amesema taifa
lipo katika kipindi Kigumu hivyo kuwataka maaskofu na wachungaji wa
makanisa mbalimbali nchini kuiombea nchi yetu ili ipate kiongozi mwenye
sifa zinazotajwa katika Biblia.
Akizungumza
kwenye Hotel ya Victoria Palace katika Hafla ya chakula cha usiku kwa
maaskofu na wachungaji wa makanisa mbalimbali ya iliyoandaliwa na
Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayoshughulika na matamasha ya
muziki wa Injili na sanaa, alisema ameamua kusema hayo mbele ya
Maaskofu na Wachungaji ambao aliwaita watu wazito wenye kuaminiwa na
kuheshimiwa katika jamii.
Hafla hiyo iliudhuriwa na Askofu Zenobius Isaya ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo mkoa wa Mwanza, Askofu
Alex Mwakisumbwa mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentokosti (P.C.T) pamoja
na Askofu Charles Sekelwa ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa makanisa ya
Kikristu mkoani Mwanza.
“Taifa
linapita katika kipindi kigumu, linajaribiwa linapita kwenye wakati
mgumu, ….Ndugu zangu yakusema yapo mengi, lakini nadhani tuzungumze
machache yanayohusu nchi yetu na Taifa letu, kwa sababu wote ni
watanzania hapa na wote tuna hamu ya kujua na kutafakari mustakabali wa
nchi yetu, umoja wetu, amani yetu na utulivu wetu,” alieeleza.
Alisema
nchi yetu inahitaji kuponywa, ili ianze upya (Reset) na kubainisha kuwa
katika kuanza upya kama Taifa linahitaji aina ya viongozi wenye sifa za
kama za viongozi wa dini ambazo zimebainishwa ndani ya Biblia na jukumu
hilo kuhakikisha akiongozi wa sifa hizi anapatikana wqanalo wachugaji.
“Taifa lipo katika changamito kama rushwa, wizi, ubakaji, kumomonyoka kwa maadili na ninyi viongozi wa dini mnaziona na kukabiliana nazo kila
siku, jamii yetu hii kwa sasa uongo umzidi, ubakaji umezidi, wizi
umezidi mauaji yamezidi sasa nini kinaendelea na kutokea na kwa nini
maovu yanaongezeka juu yetu?” alihoji Makamba.
Alisema
katika hali kama hii kuna kipindi Mungu hukasirika na kutoa adhabu,
hivyo kutaka Gharika pamoja na Sodoma na Gomola zilikuwa ni adhabu za
Mungu kutokana na watu kupitiliza katika maovu hivyo adhabu ya kwanza
ilikuwa ya Maji na ya pili ilikuwa Moto, hatujui inayofuata kwa nchi
yetu itakuwa ya nini, japo kama Taifa hatutegemei kufuka huko.
Alieleza
kwamba moja kati ya ujumbe wake kwa viongozi hao ni kama kizazi cha
sasa ama taifa tunahitaji uponyaji wa hali ya juu na kwamba katika
uponyaji huo viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa sana ya kuiponya nchi
hii ili iepuke adhabu kama za nyakati hizo zilizotolewa na Mungu.
“Shughuli
za siasa zimeingiliwa na Matapeli, lakini hata shughuli yenu pia
imeingilia na matapeli vilevile sasa tunapotafuta uponywaji wan chi yetu
ninyi mnanafasi kubwa sana kwani uponyaji tunaoongea ni wa maovu ya
kiroho, uongo ubakaji na vitu kama hivyo, ninyi mnanafasi kubwa sana.
Viongozi wa siasa pia tunayo nafasi wote tunanafasi lakini ili
tufanikiwe na nchi ipone lazima viongozi wa siasa wawe wasafi,”
alieleza.
Alisema
Askofu ama mchungaji akihubiri anapaswa kuwa msafi, na hata katika
uongozi wa siasa anaposimama mtu na kusema yeye ni jawabu la matatizo ya
wananchi ama yeye ni nyezo ya matatizo ni vizuri kumtazama sura yake
kama ameacha (maovu).
Tunapoomba
uongozi wa kisiasa zipo sifa kwani tunaomba kuongoza watu wa mungu
ambao ni wale wale wanaokuja Makanisani ndiyo wanaokuja katika siasa,
kuongoza watu wa mungu siyo kitu kidogo maana hata mamlaka ya serikali
yametambuliwa hivyo lazima vigezo vya kuongoza watu hawa view vikubwa
sana.
“Katika Biblia zinataja sifa za mtu atendae kazi ya Askofu ngoja nizisome (1 Timotheo 3.1) zinasema
… mtu akitamani kazi ya Askofu, atamani kazi nzuri. Basi, imempasa
askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi,
anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. Asiwe mlevi,
wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha,” alisema na
kuongeza katika siasa hatutafuti askofu lakini ni lazima sifa zifanane
na hizi za askofu na kuwataka viongozi hao wa makanisa kuzisoma sifa
hizo kila watu wanapopita kwao kutafuta uongozi wa nchi na kila mtu
anayetafuta uongozi lazima ajipime kwa sifa hizi.
Alisema
hata hivyo kumekuwa na mjadala mkubwa wa sifa za uongozi kuhusu kijana,
uzoefu na kubainisha kwamba amekuwa akitoa mwito kwa vijana ambao
hawana makandokando washiriki na kujitokeza katika kusaidia nchi ipone.
Makamba
aleleza vijana wengi wamekuwa waoga waoga, wengi wamekuwa wakidai
kutokuwa na fedha, uzoefu lakini maaskofu na wachungaji wanapaswa kuwa
mashahidi kupitia vitabu kwani katika Yeremia imeelezwa jinsi Mungu
alivyompatia unabii Yeremia ambaye alidai yeye bado mdogo na siwezi.
“Yeremia
alipopewa unabii alilalamika mimimi mdogo mimi siwezi, lakini mungu
alimwambiaje, ngoja nisome, (Yeremia 1: 4-10) ….Kabla sijakuumba ndani
ya tumbo la mama yako nilikujua, kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi
maalumu, nilikuweka uwe nabii kwa mataifa,” alifafanua na kuongeza kuwa
bwana alimwambia “Usiseme, ‘mimi ni mtoto mdogo. Utakwenda popote
nitakapokutuma na kunena lo lote nitakalokuagiza, usiwaogope, kwa maana
niko pamoja nawe nikuokoe.”
Kutokana
na kauli hiyo ya Januari Makamba Askofu Jacoub Lutabija alisema
amepokea ujumbe mzito ambao atakwenda kuutangaza kwa waumini wake Musima
na kubainisha kwamba kwa ujumbe huo watu wenye hekina zao wametambua
nini wanapaswa kufanya.
“Haya
ni maneno mazito, mimi nimefurahi sana na nimueleze mgeni wetu
nitakwenda Musoma kuwaeleza watu wangu juu ya ujumbe huu wenye maana
sana kwa mustakabali wan chi yetu,” alisema.
Kwa
upande wake Bahati Bukuku msanii wa Nyimbo za Injili, yeye aliwaasa
wachungaji kuacha kuomba na kufunga mambo yanapokuwa mabaya kwani tatizo
linaanzia pale maono yanapopuuzwa hivyo kuwataka kuangalia namna ya
kuunga mkono kauli zenye maono kama hayo ambayo yanasaidia kuokoa nchi.
No comments:
Post a Comment