Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, May 4, 2013

WAASI WA M23 WATOA VITISHO VIKALI KWA TANZANIA KWA MARA YA PILI



Kuptia Tovuti ya kijamii ya Twitter Jeshi la waasi wa nchini DRC kimetuma ujumbe wa vitisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, kufuatia kauli aliyoitoa Bungeni leo kuhusu Tanzania kupeleka jeshi lake DRC kukabiliana na waasi hao.
Ni hii ndio tweet yao
M23 Congo RDC ‏@m23congordc 16h @ Bernard Membe tunasubiri majeshi yako Congo. Usidaganye bunge lako eti Tanzania inakuja zima moto,bali munakuja kuweka mafuta kwenye moto.NA MPEKUZI

KABURI LA KANUMBA LAGEUZWA KITEGA UCHUMI, SASA UKITAKA KULIONA NI LAZIMA ULIPE TSHS 5,000/= KWANZA..!



KATIKA kile kinachoonekana kwamba ni wizi mtupu, baadhi ya vijana wanaojifanya kutunza Makaburi ya Kinondoni wamebuni njia ya kuwaibiawatu kwa kutumia kaburi la nguli wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba.Vijana hao hujipatia kipato kwa kuwatoza watu wanaofika makaburini hapo shilingi 5,000 kwa ajili ya kuliona na kupiga picha na kaburi la nguli huyo.  Utafiti uliofanywa na Risasi Jumamosi umebaini kwamba wageni wanaotoka nje ya Dar ndiyo wanaoongoza kwa kulizwa zaidi.
Sosi wetu ambaye naye alilizwa, alisema kuwa alishangazwa kwa kutozwa fedha na vijana hao lakini hakuwa na budi kufanya hivyo yeye na wenzake ili kutimiza lengo la kulitembelea kaburi hilo la kipenzi chao.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili liliunda kikosi kazi cha waandishi wake na kwenda kuwanasa vijana hao.







WAANDISHI WATINGA MAKABURINI

Alhamisi iliyopita, waandishi wetu walifika katika Makaburi ya Kinondoni na kukutana na jamaa kibao waliokuwa wakijishughulisha na kazi za ujenzi wa makaburi na kupanda maua ambapo walimchagua mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Mdenmark ili kuongea na wageni nao.



WAPANGA DAU

Baada ya kuwaita chemba, jamaa huyo alianza kuwapiga somo waandishi wetu na kuwaambia kwa kuwasaidia wampe shilingi 5,000 ili kuwaonesha kaburi na kuwapa historia ya marehemu tangu enzi za uhai wake mpaka alipokutwa na umauti huku akiwatahadharisha wafanye jambo hili kuwa siri.



MCHEZO WAMALIZWA

Baada ya kukubaliana kiasi hicho cha fedha, waandishi walimpatia Mdenmark kiasi cha fedha na akachukua jukumu la kuwapeleka mahali lilipo kaburi hilo. 
Wakiwa kaburini kwa Kanumba, waandishi wetu kwa kutumia ustadi mkubwa walifanikiwa kumpiga picha tapeli huyo akiwaelekeza mambo kadhaa juu ya marehemu na picha nyingine zikimuonesha akipokea fedha kutoka kwa waandishi.

TAMKO LA MHARIRI
Si sawa kulipa fedha kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba, mara kadhaa waandishi wetu wamemsikia mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa akisema kuwa hafahamu mradi huo.
Ni jukumu la Jeshi la Polisi chini ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova kuwanasa wajanja hao.

KWA WALE WAPENZI WA LINEX, HII NDO NJIA YA KUMPIGIA KURA KATIKA TUZO ZA KTMA.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2I7H4q_gXiwIW9c-h8ruJCqL0oeTN5jFcghP1tf1NB0Qmw9ptXP7wGfUNL9AhizoIBssEn6WDOVZ6FK9m4YbnmDcyhm8DXDgN8yz4NyloM8bMUpKFf1pyYALDZO8nmyXb8PZbYO9Ym_qL/s400/linex.jpg 
Kumpigia kura linex Sunday kama
Msanii bora wa kiume (bongo fleva) AF4 to 15345

Mtunzi bora wa mashairi(bongo fleva) AU4 to 15345

Msanii bora wa kiume, AB3 to 15345

Wimbo bora bongo pop BP1 to 15345

Kura yako ni muhimu.

NGOMA YAZIDI KUA NZITO KWA LADY JAYDEE, BARNABA NA LINAH WAZINGUA KUTUMBUIZA SHOW YAKE. BARNABA NA LINAH WAFUNGUKA

Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo. Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo. “Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.” Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine. Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba. Wasikilize zaidi hapa. source bongo 5

MFANYA BIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA AFARIKI DUNIA


Mfanyabiashara Costa Shrima Aliyejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam alifariki  jana muda mfupi baada ya tukio hilo.
Mfanya biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam  na tukizipata tutakuhabarisha mapema. 
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi 
Amina

NAMSHANGAA DIAMOND MIMBA IPI KWANZA...HII NI KAULI YA VJ PENNY SOMA HAPA STORY NZIMA.




Mwanamziki anayefanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ siku za nyuma alitoa kauli ya kuwa mchumba wake ambaye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki kama utakuwa mfutaliaji mzuri wa story zetu basi utakuwa umeshaisoma hii sasa Penny ameifungukia kauli hiy
Baada ya penny kulizwa juu ya ujazito wa Mwanamziki Diamond alioneka kushangzwa sana na kauli hiyo na kupaniki ghafla
Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajawah kuulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Na hivi ndivyo ilivyo kuwa katika maongezi na mwandish kutoka GPL
Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?uhusiano wangu na Diamond unaninyima raha kutokana na maneno ya watu.
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.
source bongoclantz

MAYWEATHER ULINGONI LEO KATIKA PAMBANO LA KWANZA TANGU ATOKE JELA



BAADA ya mwaka mmoja nje ya ulingo na miezi miwili jela, bondia bora kabisa duniani, Mmarekani Floyd Mayweather anarejea ulingoni usiku wa leo kwenye ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas.
Pambano lake la mwisho alipigana na Miguel Cotto na kushinda na leo atapambana na Robert Guerrero, ambaye mwenyewe anajiita The Ghost, yaani Mzimu katika uzito wa Welter Raundi 12. 
Fighting shape: Floyd Mayweather weighed in one pound under the welterweight limit at 146lbs
Yuko sawa: Floyd Mayweather alionekana yuko sawa wakati wa kupimzika uzito 
The challenger: Southpaw Robert Guerrero is the underdog
Face off: The two fighters are to meet at the MGM Grand in Las Vegas
Utaona: Mabondia hao wakitambiana wakati wa kupima uzito
Entourage: As usual, many others surrounding the two fighters
Hunitishi: Mabondia wakitunishiana vifua wakati wa kupima uzito
 
Pambano la Mayweather na Guerrero litaonyeshwa live na BoxNation kupitia Sky Channel 437 na Virgin Channel 546 kuanzia saa 7.30 usiku wa leo sawa na saa 9:30 kwa saa za Tanzania.

BREAKING NEWZZ : AJALI MBAYA IMETOKEA SASA HIVI SEGEREA KATI YA PRADO NA LORI LA MAFUTA!!


NDEGE ZA PRECISION AIR ZAPIGWA 'STOP' KURUKA AU KUTUA ZANZIBAR.


Moja ya ndege za Precision Air ikiwa angani katika moja ya safari zake.
Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB), imetoa amri ya kuzuia kutua na kuruka kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, kutokana na kutolipa zaidi ya Sh bilioni 37.2 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ada ya huduma ya uwanja wa ndege.

Amri hiyo iliyopatikana jana, imetolewa na Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar, Abdi Faki, Aprili 25 mwaka huu kutokana na malimbikizo hayo.
“Chini ya kifungu cha 43(1) cha taratibu na udhibiti wa kodi cha mwaka 2009, mimi Abdi Faki, Kamishna wa Bodi ya Mapato ninatoa amri ya kuzuia kuruka na kutua kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kuanzia saa saba usiku wa Aprili 25 mpaka hapo watakapolipa fedha hizo.”
Mbali na amri hiyo, pia ZRB inakusudia kufunga ofisi zote za kampuni hiyo zilizopo Zanzibar.
Faki alisema kuwa Precision Air Service Co. Ltd, imeshindwa na kupuuzia kulipa deni la zaidi ya Sh milioni 144.8 na zaidi ya dola za Marekani 347,066 (zaidi ya Sh milioni 520.6), kama malipo ya makato ya huduma za viwanja na usalama kwa miezi mitatu tangu Januari hadi Machi mwaka huu.
Alisema pia kampuni hiyo imeshindwa kulipa zaidi ya Sh milioni 70.5 na zaidi ya dola za Marekani milioni 1.6 (zaidi ya Sh bilioni 2.5), kama fedha za adhabu kutokana na ucheleweshwaji wa malipo kuanzia Februari hadi Agosti mwaka 2012.
“ZRB imekuwa ikiwakumbusha Precision Air Service Co. Ltd mara kwa mara ili kulipa deni hilo, lakini wameshindwa na kupuuzia suala hilo. Sheria inatutaka kufuata utaratibu wa kukusanya na kulinda mapato ya Serikali,” alieleza.
Faki alisema Precision Air iliteuliwa na Waziri wa Fedha kukusanya malipo ya huduma na usalama kwenye uwanja za ndege wa kimataifa wa Zanzibar, chini ya kifungu namba 2 ya mwaka 1999 na sheria namba 34 ya mwaka 2007.
Alisema tabia ya makusudi ya kupuuza na kuacha kufanya mawasiliano ya kiofisi na kutolipa malipo ya ada, inayofanywa na kampuni hiyo, ni uvunjwaji wa Sheria ya Ukusanyaji wa Mapato ya mwaka 2009, gharama za huduma za ndege ya mwaka 1999 na gharama za huduma ya uwanja na wakala wa usafirishaji ya mwaka 2007.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana, alipoulizwa alisema sio kweli kuwa ndege zao zimefungiwa.
“Sio kweli kuwa ndege zetu zimezuiliwa kutua na kuruka Zanzibar. Mpaka muda huu ninaozungumza nawe (saa 11 jioni) kuna ndege yetu inajiandaa kuruka kutoka Zanzibar,” alisema Ndekana.
Kuhusu kudaiwa zaidi ya bilioni 37.2, Ndekana alisema hana taarifa na kuongeza kuwa hilo ni suala la watu wa fedha na kuahidi kulitolea ufafanuzi zaidi.

source zero99,THECHOICETZ.COM

TAZAMA PICHA ZA MACHANGUDOA WANAVYOLALA MARA BAADA YA KAZI

 

Hii ni picha ikiwaonyesha madada poa walioamua kukodisha chumba kimoja kwa ajili ya kukabiliana na ugumu wa maisha jijini dar es salam,Katika picha hii ni namna madada poa hao walivyojilaza aubuhi mara baada ya kurudi kutoka kwenye shugulu zao na kujiuza

Wanawake Maarufu 60 Africa 2013: Elsie Kanza mtanzania pekee!


Elsie Kanza


MEDIA AND CULTURE


  • Dambisa Moyo - Writer, economist
  • Angelique Kidjo - Musician, Activist. Benin
  • Biola Alabi - Managing Director, MNET Africa
  • Chimamanda NgoziAdichie - Author
  • Isha Sesay - Anchor, CNN
  • Julie Gichuru - Journalist. Kenya
  • Khanyi Dhlomo - Founder, Destiny Magazine
  • Mariam Doumbia - Musician
  • Oumou Sangaré - Musician. Mali
  • Patricia Amira - Talk Show Host. Kenya
  • Yvonne Chaka Chaka - Musician. South Africa
  • Tsitsi Dangarembga - Novelist, screenwriter. Zimbabwe





FASHION AND ENTERTAINMENT

  • Iman - Model, Philanthropist, Businesswoman
  • Alek Wek - Model, Philanthropist. South Sudan
  • Bethlehem Tilahun Alemu - Founder, Sole Rebels. Ethiopia
  • Charlize Theron - Actress, Philanthropist. US/South Africa
  • Folake Folarin-Coker - Founder, Tiffany Amber. Nigeria
  • Gabourey Sidibe - Actress. US/Senegal
  • Genevieve Nnaji - Actress. Nigeria
  • Lisa Folawiyo - Founder, Jewel by Lisa. Nigeria
  • Liya Kebede - Model, Philanthropist
  • Magatte Wade - Entrepreneur. Senegal
  • Thandie Newton - Actress. UK/Zimbabwe



BUSINESS AND TECHNOLOGY

  • Bridgette Radebe - Exec Chairperson, Mmakau Mining, SA
  • Divine Ndhlukula - Founder, Securico, Zimbabwe
  • Eva Muraya - Co-Founder, Color Creations Group. Kenya
  • Eleni Gabre-Madhin - Economist and CEO, Eleni LLC. Ethiopia
  • Isis Nyongo - Managing Director, InMobi Africa. Kenya
  • Julie Ehumian - Country Manager, Google Nigeria
  • Nonkululeko Nyembezi-heita - CEO, ArcelorMittal
  • Ory Okolloh - Policy Manager, Google Africa. Kenya
  • Precious Moloi-Motsepe - Chairperson, African Fashion Itnl
  • Rebecca Enonchong - Founder and CEO, AppsTech. Cameroon
  • Wendy Ackerman - Non-Exec Director, Pick n Pay Holdings
  • Wendy Luhabe - Entrepreneur. SA



FINANCE

  • Lisa Opoku-Busumbru - COO, Goldman Sachs
  • Cathy Echeozo - Managing Director, GT Bank
  • Bernadine Okeke - EVP / Head of Private Banking, First Bank
  • Bola Adesola - Managing Director/CEO, Standard Chartered
  • Genevieve Sangudi - Managing Director, Carlyle Group Africa
  • Gugu Msibi - Senior Partner, Ernst & Young
  • Linah Mohohlo - Governor, Bank of Botswana
  • Maria Ramos - CEO, ABSA Group
  • Minoush Abdel-Meguid - Co-Founder, Union Capital
  • Ngozi Iweala Okonji - Minister of Finance. Nigeria
  • Pearl Esua-Mensah - Deputy MD, UT Bank
  • Tsega Gebreyes - Managing Partner, Satya Capital
  • Yvonne Ike - CEO West Africa, Renaissance Capital



PHILANTHROPY AND ADVOCACY

  • Graca Machel - Humanitarian, Mozambique
  • Ellen Johnson Sirleaf - President of Liberia
  • Elsie Kanza - Head of Africa, WEF. Tanzania
  • Fatou Bensouda - Chief prosecutor, Intl Criminal Court. Gambia
  • Hadeel Ibrahim - Philanthropist
  • Jeanette Kagame - 1st Lady of Rwanda
  • Joy Phumaphi - VP, Human Development Network, World Bank
  • Joyce Banda - President of Malawi
  • Leymah Gbowee - Activist, Liberia
  • Dr Mamphela Ramphele - Activist, Academic, Businesswoman
  • Toyin Saraki - Founder, Wellbeing Foundation Africa. Nigeria
  • Nkosazana Dlamini Zuma - Chair, African Union Commission

VOTE FOR STAMINA KILI AWARDS

TISA WANASWA KWA KUMKATA MKONO ALBINO



Polisi katika Mkoa wa Rukwa likishirikiana na Polisi wa Tabora pamoja na kikosi kazi maalumu cha kitaifa, limefanikiwa kuwatia nguvuni watu tisa waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kumkata mkono, Mwigulu Matonange(10) mlemavu wa ngozi Februari 15 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda
mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu(29),Nickon Kadogoo(25), Peter Msabato(32),Ignas Sungura(27),Faraja Mwezimpya (31) pamoja na Kurwa Hamis (29) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji ha Ilemba Rukwa.
Aliwataja watuhumiwa wengine ambao ni Hamis Mnywanywa ambaye ni mganga wa jadi na mkazi wa Karema Katavi,James Paskali(24) mkazi wa majimoto, pamoja na Ibrahimu Tella(27) mkazi wa kijiji Masanula-Usule Shinyanga.
Kamanda alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifuatia uchunguzi wa kina uliokua unafanywa na polisi hao kupitia mawasiliano ya simu na taarifa mbalimbali za kipelelezi ambapo siku ya April 22 walifanikiwa kumnasa Nickon Kadogoo akiwa Katavi na mkono huo akiupeleka mkoani Tabora ambapo angepata soko.
Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye na wenzake hao waliagizwa mkono huo na mganga wa jadi aitwaye Rashid Manywanywa, ambapo aliwaahidi angemlipa kila mmoja Sh600 milioni kama wangempelekea mkono huo.
Alisema baada ya tukio la kumkata mtoto huyo mkono na kumpelekea mganga huyo alidai kuwa hana fedha zote hizo kwani wao walishindwa kutumia akili kwa kuwa hata yeye ni maskini angelipata wapi fedha zote hizo, hivyo hawezi kununua mkono huo.
Baada ya kuona soko limeshindikana ndipo walipoamua kufanya mawasiliano na watu wengine na kuhakikishiwa katika Mikoa ya Tabora na Shinyanga kuna soko la uhakika ndipo safari ya kuelekea huko ikaanza.
Kwa upande wake, mganga huyo wa jadi alikiri kuwaagiza watuhumiwa hao mkono huo na kudai kuwa alitaka kutumia kutengenezea chombo cha usafiri ambacho alidai kuwa ni ungo ambao unatumika na wachawi kusafiria nyakati za usiku.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 04.05.2013 VICHWA VIKUBWA LEO MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAFUTWA,AJALI YA BASI YAUA 7 NA NYARAKA ZA KUHUJUMU KATIBA ZAKAMATWA.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.NA MILLAD

Ruge Mutahaba kumjibu Lady Jay Dee Jumatatu


Kwenye kipindi cha Power Breakfast kitakacho rushwa siku ya jumatatu saa mbili asubuhi Ruge Ataongelea issue ya Jay Dee ,Lady Jay Dee ameingia kwenye vita kali na Clouds Fm huku akimshambulia Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kwa madai kuwa ndio wanaokula jasho la wasanii.

Ughaibuni si shwari ! Nani kachonga deal la kuibiwa kamanda Ras Makunja wa FFU ?



Watu wasio julikana wafanikiwa kuiba ndege wa Kamanda Ras Makunja !
Moja ya ndege wake amepatiaka katika kituo cha ifadhi ya wanyama !



Kamanda anamlaumu jirani kuwa ndie alichonga deal!

Na mpekuzi wa habari ughaibuni,

Habari za uhakika zimevuja kuwa mkuu wa bendi hisiyo kaukiwa na  virungu "Ngoma Africa band" aka FFU kule Ujerumani ,kamanda wao Ras Makunja amejikuta akishika kichwa baada ya watu wasio julikana kuingia katika imaya yake kuvunja moja ya matundu yaliokua na ndege aina bundi jirani ya nyumba 
na kutoweka nao ! inasemekana kamanda na familia yake walikua hawapo nyumbani,na wajanja awakatumia nafasi hiyo.

Kamanda Ras Makunja alishikwa na butwaa baada ya kugundua kuwa kwenye chumba kilichokua na ndege aina bundi mlango uko wazi na ndani hakuna ndege!

Baada ya kuenda kurepoti Polisi ikagundulika kuwa Bundi wawili wa kamanda walichukuliwa na idara ya kuifadhi wanya ya Ujerumani,kwa madai kuwa ndege hao walikua wakubwa mno na chumba chao ft 12X12 hakitoshi.
Kwa kupitia wakili wake mkuu wa kikosi kazi kamanda Ras Makunja ameambiwa bora awaruhusu ndege hao warudishe katika nchi za joto walikotoka,
Bundi hao walikua katika imaya ya mwanamuziki huyo kama ndege wa kufuga nyumbani,ambao alipewa na moja wa marafiki zake miaka ya nyuma.

Moja wa majirani wa kamanda Ras makunja ndiye anayetupiwa lawama na kamanda huyo kuwa awapendi ndege hao aina ya bundi, na jirani naye anarudisha
lawama kwa kudai labda baadhi ya wanafamilia ya kamamnda ndio waliotengeneza fitina ya kuondolewa kwa bundi hao,kwani walikuwa wanatisha.
Mwanamuziki kamanda ras Makunja anatafuta mbaya wake aliyesabisha kuchukuliwa kwa bundi wake ambao ana kibali cha kuwamiliki katika imaya yake ya Anunnaki Empire.
Tunampa pole kamanda ras makunja kwa yaliyomkuta.