Mahmoud akiwa na binti yake wakati wa kampeni zilizofanyika jana uwanja wa Bustanini.
Mgeni rasmi wa leo Alhaj Mwangi Kundya |
Na Andrew Chale, Zanzibar
CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 29, kinatarajia kufanya kampeni
yake ya Saba (7) ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la uwanja wa tawi la
CCM, Mbweni, Kiembesamaki, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Kiembesamaki, ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa,
Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini, Alhaj Mwangi Kundya.
Akielezea mkutano huo wa Saba, mapema leo, unaotarajiwa kuwa majira ya
Saa kumi jioni, eneo hilo la CCM Mbweni, Mahmod Thabit Kombo ,
aliwaomba wananchi wa wa Kiembesamaki kufika kwa wingi kwenye mkutano
huo, ambapo pia kutakuwa na shamrashamra mbalimbali zitakazoanza majira
ya Saa Nane, mchana. Hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi
ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.
“Leo Januari 29, nawaomba wananchi wa Kiembesamaki, kujitokeza kwa
wingi eneo la CCM Mbweni, ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu
tuliyojipangia ndani ya chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.
Aidha, aliwaomba wananchi wa Jimbo hilo, ifikapo Februari 2, 2014 siku
ya Jumapili, kumpa kura za NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda
kuwatetea Bungeni kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza
kero zinazowakabiri.
No comments:
Post a Comment