Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 19, 2014

HII NDIO RANGE ANAYOSUKUMA MWANADADA LADY JAYDEE KWA SASA

 
Hahaaaa kweli wanaosema wasanii wabongo si wote wenye njaa kama wengi tuzaniavyo, ni juzijuzi tu hapa msanii Diamond Platnumz kavuta mkoko aina ya Toyota Land cruiser V8.
Sasa mwanadada Lady Jaydee na e kaamua kujibu mapigo kwa kuonyesha mkoko wake mpya aina ya Range Rover Evoque ambayo nayo pia ni ya bei mkasi lakini bado hajamfikia Diamond. Katika tafutatafuta yetu mdakuzi wa Bongoclan alifanikiwa kupata bei za gari hilo kwa nje ya nchi, ambayo kama ni jipya ni kama dola za kimarekani 45,000 ambazo ni sawa na shilingi za ktanzania milioni 72,495.000 na kama limetumika ni kama dola za kimarekani 42,000ambazo ni sawa na 67,662,000.

Kwa msanii kama Lady Jaydee na Diamond kumiliki magari ya gharama kama hayo ni uthibitisho tosha kua mziki wa Bongo flava unalipa sana kama wasanii wataamua kufanya mziki kama kazi na si masihara. Ni ukweli usiopingika kua wasanii hawa wawili wameweza kua mfano bora kwa jamii kwani mshiko wanaopata wameutumia kuwekeza katika biashara mbalimbali ambazo zimewafanya kuacha kutegemea pato la mziki peke yake.CHANZO BONGOCLAN

CHANZO BONGOCLAN TZ

No comments:

Post a Comment