MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mara imemsomea mashitaka ya kuharibu
mali Diwani wa Kata ya Kigera Gabriel Ocharo(CUF) zenye thamani ya
shilingi milioni 25,300,000 kinyume na kifungu cha 326 ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Imedaiwa
na Mwendesha mashitaka Jonas Kaijage mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mwandamizi Faisal Kahamba Diwani huyo kinyume na kifungu hicho
alishiriki uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule ya msingi
Kigera A mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ilielezwa
na mwendesha mashitaka kinyume na utaratibu,Diwani huyo alitenda kosa
hilo la uharibifu wa majengo ya madarasa ya shule hiyo na kupelekea
kufanya wanafunzi kushindwa kuhudhuria vipindi madarasani.
Kutokana
na kushindwa kukidhi masharti ya dhamana kulingana na thamani ya
uharibifu uliofanyika katika shule hiyo,Diwani Ocharo alipelekwa rumande
hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena februari 2 mwaka huu.
Hivi
karibuni katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halimashauri
ya Manispaa ya Musoma lililofanyika chini ya Naibu Meya wa Halimashauri
hiyo Bwire Nyamwero(Chadema) lililotoa agizo kwa Afisa Elimu Msingi wa
Halimashauri hiyo kutoa
taarifa polisi juu ya uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule
ya
msingi Kigera A uliodaiwa kufanywa na Diwani huyo.
Kwenye kikao hicho, Diwani wa Kata ya Bweri Zidi Sondobhi(Chadema)
alisema katika muhula huu wa masomo wanafunzi wa shule ya msingi Kigera
A wameshindwa kuhudhulia vipindi madarasa kwa kile kilichoonekana
majengo sita ya shule hiyo kung'olewa mabati na kushindwa kuezekwa hali
inayofanya wanafunzi kushindwa kusoma na kuwaaomba madiwani watoe tamko la kumtaka Diwani huyo akamatwe.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya
Manispaa ya Musoma Ahmed Sawa alilieleza Baraza hilo hakuwa na barua yoyote wala kutoa maagizo ya
kuondolewa mabati ya shule hiyo hali iliyomfanya Naibu Meya kuomba
maelezo ya kina kutoka kwa Diwani wa Kata husika juu ya uhalibifu
uliofanywa kwenye shule hiyo na baadae kutoa amri ya kufunguliwa mashitaka.
HABARI KWA HISANI YA SHOMARY BINDA
HABARI KWA HISANI YA SHOMARY BINDA
No comments:
Post a Comment