Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda akiongea
na waandishi baada ya kushinda kesi katika Mahakama ya Hakimu mkazi
Kisutu.
Meneja
Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL),
Theophil Makunga akiongea na wanahabari baada ya kushinda kesi Mahakama
ya Hakimu mkazi Kisutu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd,Tido Mhandoa kiongea na waandishi wa habari baada ya hukumu.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo imetoa hukumu ya kesi
ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja
Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL),
Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson
Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima
ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006),
Absalom Kibanda ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa
mashitaka kutojitosheleza. (PICHA: DEOGRATIUS MONGELA NA NYEMO CHILONGANI/GPL)
No comments:
Post a Comment