Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
WIMBI la ubakaji wa watoto wadogo limeendelea, baada ya watu wawili
kuripotiwa kuwabaka wasichana wadogo wa kike katika matukio mawili
tofauti wiki iliyopita.Mtoto aliyebakwa.
Huko Mbagala Zakhem, jijini Dar, kijana aliyefahamika kwa jina moja la
Robert alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka tisa baada ya kumnywesha bia
na baadaye kumchoma kwa kisu chenye moto katika harakati za kulazimisha
kitendo hicho.
Mama mzazi wa msichana huyo, Neema Mohamed, aliliambia gazeti hili kuwa
Alhamis iliyopita mtoto wake hakurudi nyumbani baada ya kuondoka na
msichana aitwaye Anna, ambaye ni jirani yao aliyemuomba mapema
amsindikize saluni kwa ajili ya kusuka.
“Nilihangaika sana kumsaka mwanangu, yule dada akawa anakataa kwamba
hajui alipo wakati yeye ndiye aliondoka naye, nikatoa taarifa Kituo cha
Polisi cha Mbagala Maturubai, juhudi zikazaa matunda kwa kumpata
mwanangu na mtuhumiwa. Anna alipanga njama na Robert,” alisema.
Mtoto huyu naye alibakwa.
Mtoto Neema naye alikiri kufanyiwa unyama huo usiku wa manane na
watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Mbagala
Maturubai kwa hati yenye kumbukumbu MBL/RB/426/2014, KUBAKA.
Wakati huo huo, mtoto mwingine aitwaye Prisca ambaye pia ana umri wa
miaka tisa, mkazi wa Kongowe Mzinga mkoani Pwani, naye alifanyiwa unyama
kama huo na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 anayefahamika maeneo hayo
kama Anko.
Mama wa mtoto huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema awali hakuwa
akifahamu chochote hadi pale alipoelezwa na marafiki wa binti yake huyo
kuhusiana na tukio hilo lililotokea Desemba mwaka jana.
Prisca aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, alipita jirani na
nyumba ya Anko huyo aliyemuita na kumtuma vocha dukani, lakini
aliporejea na kuingia sebuleni akabakwa
Mtuhumiwa huyo anatafutwa na jeshi la polisi kwa jalada la kesi MBL/RB/14111/2013 KUBAKA.
CREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment