Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 21, 2014

Iran kutohudhuria mazungumzo ya Syria-UN

Ban-Ki-Moon_1932746c_32221.jpg
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amefutilia mbali mwaliko uliotolewa kwa Iran kuhudhuria mazungumzo ya amani ya Syria nchini Uswisi.
Msemaji wa Ban Ki Moon, alisema Katibu Mkuu huyo alichukua uamuzi huo kwasababu Iran, ilikataa kutoa ahadi ya wazi kwamba inaelewa na inaunga mkono hatua ya kuundwa kwa serikali ya mpito Syria, licha ya kutoa ahadi zisizo rasmi kuhusu hilo.
Umoja wa Mataifa umelazimika kufutilia mbali mwaliko wake kwa Iran uliokuwa umeitaka nchi hiyo kuhudhuria kongamano linalonuiwa kutafuta Amani ya Syria.
Sababu kuu ni kwamba Iran, ilikataa kuunga mkono pendekezo la kuwa na seriali ya mpito nchini Syria.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nesirky amedokeza kuwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesikitishwa sana na uamuzi huo wa Iran uliokataa pendekezo la serikali ya mpito ambalo liliafikiwa na jumuiya ya kimataifa hapo 2012 kama njia moja ya kutafuta dawa ya mzozo wa Syria.
Lakini kwamba kikao hicho cha Amani ya Syria kitaendelea bila Iran, si ajabu Ban ki-Moon ndie aliyewashangaza wengi pale alipopeleka mwaliko huo kwa Iran na kusababisha mzozo huo wa kidiplomasia.
Wapinzai wa serikali ya Syria walikasirika na kutishia kutohudhurua kikao hicho.
Marekanii kwa upande wake ilikuwa tayari kushinikiza kuwa iwapo Iran haitakubali pendekezo la serikali ya mpito ya Syria basi isialikwe.
Huku malumbano hayo yakiendelea Iran ilikuwa imetangaza kujioindoa.
Balozi wa Iran kwa umoja wa Mataifa Mohammad Khazaee, amenukululiwa akisema Iran, inataka sana suluhu la kisiasa kwa mzozo wa Syria lakini haitakubali masharti kama kigezo cha kushiriki mazungumzo hayo ya amani.
 TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment