Mkazi wa
Mwenge jijini Dar es salaam Philimon Nelson (45) ambaye alikuwa
mfanyakazi wa GEPF amekutwa amefariki akiwa amelala kitandani chumbani
kwake, huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.
Kwa
mujibu wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam taarifa zinasema
kuwa sababu za kifo hicho bado hazijafahamika ingawaje kwa maelezo ya
ndugu wa marehemu walidai kuwa marehemu enzi za uhai wake alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
Na
kwasasa maiti imehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi huku
upelelezi ukiendelea. Na katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda
maalum ya Dar es salaam limesema kuwa mnamo januari 19,2014 saa nane
kamili mchana maeneo ya Buguruni Kisiwani maarufu kama Msikitini wa
Msufini ilikutwa maiti ya mtu mmoja mwanaume aliyetambulika kwa jina la
Shabani Rajabu , anayekadiliwa kuwa na umri wa kati ya 35 hadi 40 ambaye
ni mfanyabiashara soko dogo la Kariakoo ikiwa imelala maeneo hayo na
huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.
Aidha
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limesema kuwa kuhusu tukio
hilo kwa mujibu wa mashuda walidai kuwa mtu huyo alikuwa akitembea na
ghafla alidondoka chini na kufariki dunia .
Jeshi la
polisi kanda maalum ya dar es salaam limeendelea kusema kuwa chanzo
chake bado hakijafahamika na maiti imehifadhiwa hospitali ya Taifa
Muhimbili.
No comments:
Post a Comment