Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 19, 2014

KITENDAWILI CHA BARAZA LA MAWAZIRI KUTEGULIWA LEO?


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue

  Ikulu yafanya uteuzi, kuhamisha Makatibu Tawala
  Wamo Chambo, Dk. Ndunguru

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, leo anakutana na vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam kwa kile kinachotarajiwa kutangazwa kwa mawaziri wapya.
 
Uwezekano huo unatokana na taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana  ikieleza kuwa Balozi Sefue ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri atazungumza na wanahabari katika kikao hicho kinachotarajiwa kufanyika wakati wowote leo. 
 
“Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Balozi Ombeni  Sefue ambaye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, leo, Jumapili, Januari 19, 2014, atazungumza na waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika Ikulu, Dar es Salaam.” Ilisema taarifa  hiyo, iliyosainiwa na Mwandishi wa Rais, Salva Rweyemamu.
 
Matarajio ya wengi yalikuwa Rais Jakaya Kikwete angetangaza baraza la mawaziri wiki hii ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na mawaziri  wanne walioshinikizwa na Bunge kujiuzulu, kufuatia kushindwa kusimamia majukumu yao kwenye Operesheni Tokomeza Ujangili iliyosababisha vifo na uharibifu wa mali za watu.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIII MOTOMOTO(USIPITWEEEEE)
Waliojiuzulu ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis  Kagasheki , Waziri wa Mambo ya Ndani Dk  John  Nchini,  na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha. Pia alitarajiwa kutangaza Waziri wa Fedha kuchukua nafasi ya marehemu Dk William Mgimwa, aliyeaga dunia Januari mosi mwaka huu.
 
Mwanzoni mwa mwezi huu kumekuwa na taarifa kwenye vyombo  vya habari zikipendekeza baadhi ya sura zinazotarajiwa kuingia katika baraza hilo.
Hata hivyo, ukweli utajulikana leo baada ya Katibu Mkuu Kiongoza kutangaza rasmi.
 
Kuna wasiwasi kuwa huenda Rais akawabadilisha baadhi ya  mawaziri wanaodaiwa kuwa mizigo, baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwataja na kupendekeza wahojiwe na Kamati Kuu (CC) ya chama. 
 
Wizara zinazolalamikiwa ni ya Maji, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.
Aidha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dk. John Ndunguru, anakwenda kuwa Katibu Tawala wa  Mkoa wa Kigoma.
 
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema uteuzi huo pia umemhamisha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sipora  Liana kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za MItaa (Tamisemi) na nafasi yake kuchukuliwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma  Iddi.
 
MAKATIBU WAPYA 
Makatibu Tawala wapya wa mikoa mitano ni Wamoja  Dickolangwa (Iringa)  Abdallah  Chikota (Lindi), Symthies  Pangisa (Rukwa),  Alfred Luanda (Mtwara) na  Jackson  Saitabau ( Njombe). 
 
WALIOHAMISHWA
Beatha Swai aliyekuwa Pwani amehamia Tamisemi, Benedict Ole Kuyan zamani Tanga sasa Mara,  Salum Chima wa  Rukwa  anayekwenda  Tanga, Mgeni Baruani zamani  Njombe na  sasa anakwenda Pwani. Uteuzi na uhamisho  huo ulianza rasmi jana kwa mujibu wa  taarifa ya Ikulu.  
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment