skip to main |
skip to sidebar
Maegesho ya magari Dar sasa kusimamiwa na Jiji tu
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imezinyang’anya rasmi Manispaa
majukumu ya kusimamia maegesho ya magari na imefuta vibali vyote vya
maegesho vilivyotolewa na mamlaka hizo. Hatua hiyo imekuja baada ya
Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dar es Salaam (RCC) kuagiza halmashauri ya
Jiji kufanya kazi hiyo baada ya kubaini halmashauri za Ilala, Kinondoni
na Temeke, kisheria hazikupaswa kusimamia maegesho ya magari.
Aidha, RCC imeamua kusitisha mikataba ya usimamizi ya manispaa hizo
na kuagiza jiji lisimamie maegesho, baada ya kubaini mawakala waliokuwa
wamepewa kazi hiyo, walikuwa wakibughudhi madereva na wamiliki wa magari
kwa kuwatoza faini bila kuzingatia utaratibu, kuvizia na kukokota
magari kwa ubabe.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji, Wilson Kabwe, alisema,
“tulishapeleka malalamiko kwamba manispaa zinafanya kazi isiyo yao
kisheria. Vile vile waliokuwa wanafanya kazi hii kama mawakala, walikuwa
wanatoza faini bila utaratibu.”
Alitaja mawakala hao ni Mwamkinga Auction Mart Ltd na Tambaza Auction
Mart and General Broker, ambao katika utekelezaji, pia wanashutumiwa
kwamba wafanyakazi walitumia lugha chafu kwa wananchi, walivizia magari
kuyakamata, kuyafunga na kuyavuta kwa nguvu kupita kiasi na kutoza faini
kubwa zisizo na utaratibu.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alipoulizwa ni kwa namna gani manispaa
‘zilipora’ mamlaka ya jiji na kuanza kusimamia maegesho, alikiri kuwepo
kasoro.
“Kama wangechukua (manispaa) ikawa hakuna bughudha kwa wananchi,
yawezekana wangeachiwa. Aliyechukua ni mwenzetu, na kwa kuwa tumeona
alifanya makosa, umefika wakati wa kumnyang’anya,” alisema.
Vibali vyafutwa Katika kuanza kutekeleza majukumu, Mkurugenzi huyo wa
Jiji alisema wanafanya kazi ya kusimamia maegesho kwa kushirikiana na
wakala wake, National Parking Solution (NPS) na kwa kuanzia, vibali
vyote vya maegesho ya magari vilivyotolewa na mamlaka zingine vimefutwa.
Walio na vibali warudishe halmashauri ya jiji ili wapewe vingine kwa
mujibu wa sheria. Vibali vingine vilivyofutwa ni vya teksi,
vilivyotolewa na mamlaka zingine vimefutwa na vitatolewa upya na
halmashauri kwa kuwa baadhi ya vituo vipo katika maeneo yasiyostahili.
Pia vituo vyote vya teksi visivyo katika mpango wa jiji, vitaondolewa
kuwezesha magari kupita kwa urahisi kupunguza msongamano. Uamuzi
mwingine uliotangazwa na jiji ni kwamba maeneo yote yaliyokuwa maegesho
ya magari, ambayo yamegeuzwa kwa matumizi mengine, baada ya kukamilika
kwa ujenzi wa majengo mbalimbali katika maeneo ya katikati ya jiji na
Kariakoo, yatarajeshwa.
Vile vile magari makubwa ya mizigo kuanzia tani 3.5, yanatakiwa
kufuata sheria zilizoainishwa kuhusu kuingia kati kati ya jiji. Pia ni
marufuku kwa maguta na mikokoteni yenye mizigo mikubwa kuingia katikati
ya jiji.
Bodaboda zote haziruhusiwi kuingia katikati ya jiji, ingawa Mkurugenzi Kabwe alisema hilo watashirikiana na polisi.
Faini Wakati inadaiwa mawakala chini ya manispaa walitoza faini hadi
takribani Sh 300,000 kwa waliokiuka utaratibu wa maegesho, mkurugenzi wa
Jiji ametangaza viwango vipya vya adhabu, watakaokiuka sheria ni kati
ya Sh 20,000 na Sh 80,000 kulingana na kosa.
Alitoa mfano wa kwamba faini ya kuvuta gari lililovunja sheria, faini
yake haizidi Sh 80,000. Makosa mengine kama vile kutolipa ushuru wa
maegesho ya magari na kufunga gari, kuegesha sehemu zisizoruhusiwa,
kuingiza gari zaidi ya tani 3.5 katikati ya jiji na kuosha gari kwenye
maegesho, faini yake haizidi Sh 50,000.
Makosa mengine ambayo faini yake haizidi Sh 50,000 ni kufanya
biashara kwenye maegesho ya magari, kuweka vizuizi kwenye maegesho,
kutengeneza magari kwenye magesho na kushusha au kupakia mizigo maeneo
ya magesho bila idhini ya halmashauri.
Aidha faini ya kulaza gari lililokamatwa kwa siku ni Sh 20,000.
“Faini lazima ziwepo, lakini kupiga faini au kuvuta gari, zitakuwa
jitihada za mwisho. Lazima elimu itolewe kwanza. Wenzetu (mawakala wa
manispaa) walitoza kwa kubughudhi watu,” alisema.
Mkataba NPS Akizungumzia ushirikiano wao na NPS, Mwanasheria wa Jiji,
Robert Mageni alisema alipatikana kwa ushindani na mkataba wake unaisha
Agosti mwakani. Kwa mujibu wa makubaliano kati ya NPS na Halmashauri ya
Jiji, malipo ya faini zote zitakazotozwa, zitalipwa kwa wakala huyo na
baadaye kurejeshwa halmashauri ya jiji kwa utaratibu uliowekwa na sheria
za fedha.chanzo Habari Leo
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YEU KWA HABARI NYINGII MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment