Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 14, 2014

Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (Afrika) wakutana Dar


1Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola barani Afrika na Katibu wa Bunge la Ghana Bwana Emmanuel Anyimadu (kushoto) akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya Umoja huo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika), mwenyeji wa Mkutano huo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah. 2Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) wakiwa kwenye Mkutano  wa kamati ya Utendaji Jijini Dar es Salaam. Washiriki katika Kamati ya Utendaji wanatoka katika nchi za Ghana, Uganda, Tanzania, Botswana, Kenya, Afrika Kusini na Zanzibar. 3 
Picha ya pamoja ya Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola (Afrika) pamoja na maafisa waandamizi wakati wa Mkutano wa Kamati ya Utendaji  Jijini Dar es Salaam. Lengo la Mkutano huu ni kuandaa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Makatibu wa Bunge wa Jumuiya ya Madola  (Afrika) utakaofanyika nchini Kenya mwezi Juni, 2014. (Picha na Prosper Minja – Bunge)

No comments:

Post a Comment