![]() |
Merry Patrick au Mama Jack aliyetoweka kimiujiza |
USHIRIKINA.
Katika hali inayotafsiriwa kuwa ni imani
za kishirikina, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Merry Patrick
au Mama Jack, mkazi wa Magole B Ilala jijini Dar es Salaam, ametoweka
kimiujiza nyumbani kwake usiku wa manane wiki iliyopita.
Chacha Muhochi, mume wa mwanamke huyo,
aliliambia gazeti hili kuwa siku ya tukio, saa tisa usiku akiwa nje ya
nyumba akilinda mifugo yake, aLimwacha mkewe amelala ndani, ghafla
alisikia sauti ya mtoto wake wa mwisho akilia, hali iliyomfanya
akimbilie ndani kutazama kilichotokea.
Baada
ya kuingia ndani, alishangaa kutomuona mkewe kitandani kwani mtoto
alikuwa peke yake. Alipojaribu kuchunguza, mlangoni mwa nyumba yake,
aliona damu. Aliingia katika vyumba vyake vyote pasipo kumuona mkewe
huyo, ambaye pia alikuwa ni mwanakwaya wa SDA.
“Sikujua
nini kilimkuta mke wangu, nilihangaika kila kona sikumuona, nikaona
niende kwa mjumbe na kutoa taarifa polisi, hadi ninavyozungumza na wewe
bado hajaonekana,” alisema Chacha na kuonesha hati ya Polisi (RB)
STK/RB/23241/2013.
Lakini
katika hali ya kushangaza, baadhi ya majirani na waimba kwaya wenzake,
wanadai mwanamke huyo huwa anaonekana nyakati za usiku na kwamba simu
yake ikipigwa inaita bila kupokelewa, lakini baadaye hutuma ujumbe
usioeleweka.
Mmoja
wa waimba kwaya ambaye pia ni jirani na mama Jack, alisema wamekuwa
wakikesha katika kufanya maombi kila siku, lakini wamekuwa wakishangazwa
na ujumbe wanaopata wanapojaribu kupiga simu ambayo huwa haipokelewi.
“Tuache
kwanza, kwa sasa ana majukumu, yuko bize, ila mchawi wenu hataki akae
hapa, anaweza kuja muda wowote, yuko bomba kinoma,” huu ni mmoja wa
ujumbe unaotajwa kuandikwa kupitia simu ya mwanamke huyo anayedaiwa
kutoweka kimiujiza.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment