Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 15, 2014

Mtalii wa Demark abakwa India


Serikali imethibiti sheria za kupambana na ubakaji India
Polisi nchini India wanachunguza kisa cha mtalii mwanamke raia wa Denmark aliyebakwa na genge la watu mjini Delhi.
Inaarifiwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa amepotea wakati akirejea hotelini alikokuwa anaishi katikati mwa mji.
Polisi wanasema aliporwa kwa mabavu na kisha kubakwa akishikiwa kisu.
Duru zinasema kuwa mwanamke huyo aliondoka India Jumatano asubuhi.
Pameanza kuwa na umakini kuhusiana na visa vya ubakaji nchini India tangu mwanafunzi aliyefariki mwaka 2012 baada ya kubakwa akiwa kwenye basi mjini Delhi.
Serikali iliweka sheria kali zaidi kuhusu visa vya dhuluma za kingono mwaka jana baada ya maandamano kufanyika kulaani kitendo cha ubakaji.
Mwanamke huyo aliambia polisi kuwa aliwaomba wanaume hao kumueleka alikokuwa anaishi baada ya kupotea lakini badala yake wakambaka.
Wanaume hao walimuibia na kisha kumbaka.
Mwezi Machi mwaka jana mtalii mmoja rais wa Switzerland alibakwa na genge la wanaume katika jimbo la Madhya Pradesh.
Wanaume sita walifungwa jela maisha kwa kitendo hicho

No comments:

Post a Comment