.
Aidha Dr Kawambwa amesema mahitaji ya walimu wa masomo ya sayansi ni walimu 26,000, lakini serikali
inauwezo wa kutoa mafunzo kwa walimu 2100 wa fani hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Waziri Kawambwa
ametoa kauli hiyo wakati akizindua mradi wa kompyuta ndogo za mkononi
kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Wama Nakayama iliyopo wilayani
Rufiji, mradi unaoratibiwa na Taasisi ya Opportunity Education ya
Marekani.
Sanjari na hayo Dr Kawambwa amesema serikali ipo kwenye mkakati wa kujipanga kutumia teknolojia ili
kuwezesha wanafunzi kujifunza mambo mengine licha ya idadi ndogo ya walimu iliyopo.
No comments:
Post a Comment