Hii
ndio Baiskeli iliyokuwa imebeba Ulanzi kutoka kijiji ya Marehemu
huyo ikiwa imeegeshwa klabuni ambapo alipaswa kuuza pombe hiyo
Mama
Mkwe wa marehemu huyo Bi Alophoncena Kunzugala akiwa kando ya mwili wa
mkwe wake kulia ,kushoto ni polisi waliofika eneo la tukio
Mwili wa marehemu Erasto Ilomo aliyeanguka na kufariki dunia hivi punde
Mwili huo ukipakiwa katika gari la polisi
MFANYABIASHARA
ya ulanzi kutoka kijiji cha Luhuhu Iheme kata ya Mgama Bw Erasto
Ilomo ameanguka na kufariki dunia mara akiwa jirani kufika katika
Klabu cha pombe za kienyeji eneo la Magari mabovu kata ya Miyomboni
Kitanzini.
Tukio
hilo limetokea majira ya saa5 asubuhi ya leo wakati kijana huyo
akiwa amebakiza kama mita 15 kufika katika klabu cha pombe kuwauzia
pombe hiyo wateja wake .
Wakizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.com eneo la tukio baadhi ya
mashuhuda ambao hawakupenda kuanika majina yao kwa kuhufu kusaidia
polisi walisema kuwa kijana huyo alikuwa nyuma akiifuata Baiskeli yake
ambayo ilikuwa ikisukumwa na vijana wawili vibarua kutoka Ipogolo
kama ilivyo siku zote .
Hata
hivyo kabla ya kufika eneo la Klabu hali vijana hao wakiwa
wameifikisha Baiskeli hiyo nje ya Klabu wakisubiri kupewa ujira wao
kwa kazi ya kusaidia kusukuma Baiskeli ndipo walipoaona wananchi
wakimsaidia boss wao huyo ambae alianguka ghafla .
Walisema
kuwa jitihada za wananchi eneo hilo ambao ni wafanyabiashara ziliweza
kuonekana kwa kumnyanyua kijana huyo kutoka barabarani na kukalisha
katika ukuta wa nyumba ya jirani kabla ya kuhema kwa nguvu mara tatu
na kufariki dunia.
Mama
Mkwe wa marehemu huyo Alophoncena Kunzugala aliueleza mtandao huu
wa matukio daima kuwa hana hakika kama mkwe wake alikuwa mgonjwa
kwani hata jana alifika mjini hapa kuleta pombe hiyo.
Jeshi
la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuuchukua mwili huo kuupeleka katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
credit: Matukio daima
No comments:
Post a Comment