Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Goodluck
Jonathan wa Nigeria wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya
mazungumzo Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya
Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako walikuwa wakihudhuria Mkutano
wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………
Rais
wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria
Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika(WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.
Rais
Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili
walipokutana na kufanya mazungumzo leo, Alhamisi, Januari 23, 2014,
kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao
wanahudhuria wa Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.
Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja, Nigeria.
Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.
Nigeria
inakuwa nchi ya nne katika Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi,
mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini
mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika
Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.
Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa mkutano huo na sasa Nigeria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 January, 2014
No comments:
Post a Comment