Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na
Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa
January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi,
na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete ambaye alitua
nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara
ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la
Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo,
ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba
ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa.
Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku
akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa
Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo
January 24, 2014.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William
Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana
jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani.
Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos,
Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili
kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa
jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22,
2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa
ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo
nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment