Rais wa
Nigeria, Goodluck Jonathan, amewafuta kazi makamanda wake wakuu wa jeshi
,na kufanya mabadiliko ambapo amemteuawa mkuu wake wa ulinzi, wakuu wa
majeshi ya anga na majini .Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu hatua hiyo .
Mkuu wa mpya wa majeshi Alex Badeh, anatoka kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la
Nigeria limekuwa likihangaika kudhibiti uasi wa kundi la kiislam la ,
Boko Haram, ambalo limekuwa likiendesha harakati zake zaidi katika
maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi.
No comments:
Post a Comment