Kiungo wa Manchester United Anderson amesafiri kwenda jijini
Florence kwa ajili ya kwenda kufanya vipimo vy afya kwa ajili ya
kujiunga kwa mkopo na klabu ya Serie A ya Fiorentina.
Mbrazil
huyo amewaambia rafiki zake kwamba anataka uhamisho wa moja kwa moja ili
kujihakikishia muda wa kucheza lakini United kwa sasa wapo tayari kutoa
ruhusa ya biashara ya mkopo tu.
Anderson alitokea jijini Manchester kupitia Frankfurt leo alhamisi na anategemewa kukamilisha kila kitu kesho mchana.
Anderson amecheza mechi 4 tu katika premier league msimu huu, na nane kwa ujumla.
Alijiunga na United mwaka 2007 akitokea Porto kwa ada ya £20million, ameichezea timu hiyo mechi 179 na kuifungia mabao 9.
No comments:
Post a Comment