Chelsea
wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazimiwa na
ushindani wa hali ya juu katika mfululizo wa michuano ya kombe la FA
Cup.
Chelsea
ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika
mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.
Kocha wa
Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema,
“Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.
Roberto
Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani ya Swansea,
ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni mechi
liyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff
watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton.
Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya
Championship, Charlton FC.
Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.
Mshindi
wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati
ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe
hilo ambalo fainal yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.
No comments:
Post a Comment