Taarifa
ambazo zimetufikia kupitia kituo cha WAPO Radio FM zinaeleza kwamba
kuna bomu limelipuliwa kwenye kanisa katoliki la Mtakatifu Karoli,
Ruanga huko USA River jijini Arusha, ambapo wanakwaya takriban 6
wamejeruhiwa.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo ambazo zimetufikia, zinaeleza kwamba watuhumiwa
ni jeshi la Polisi, na kwamba walirusha kitu kinachosadikiwa kuwa bomu -
lililojeruhi 6, ambapo 4 kati yao wameruhusiwa baada ya matibabu kwenye
hospitali ya Mission na ya Wilaya ya Arumeru.
Majira
ya saa sita na nusu, waumini walidai kuona gari la polisi likipita kwa
kasi, na lilipowakaribia walistuka mlipuko ukiwarusha pembeni, ambapo
walijikuta na majeraha na usoni, mapajani na maeneo mbalimbali ya mwili.
Kisha baada ya hapo gari ilisogea mbele na kuanza kurusha mabomu kwa
watu wowote iliokutana nao.
Hadi
sasa inaelezwa kuwa uchunguzi umeshaanza kufanyika, huku Kamanda
Liberatus Sabas akikataa kuzungumzia zaidi suala hilo. Alipotafutwa na
WAPO Radio FM, hakueleza kwa kina, lakini akasema kuwa sio suala la
kwaya kama ambavyo imeelezwa, bali ni wakinadada wawili na kwamba hawezi
kuzungumza zaidi, bali kesho (Ijumaa) atatoa taarifa rasmi na iliyo
kamili kwa vyombo vya habari.
Alipoulizwa
kuwa kama ni kweli jeshi la Polisi linatuhumiwa kuhusika, alisema kuwa
atazungumza kesho kuhusiana na tukio hilo. Tukio hili limetokea ikiwa ni
siku mbili zimepita tokea kuapishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi
mpya, Ernest Mangu ambaye amechukua nafasi ya IJP Said Mwema
aliyestaafu.
Source: Gospel Kitaa.
No comments:
Post a Comment