Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu
Serikali ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake
na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa. Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu
Tanzania itakavyonufaika na mfumo wa himaya moja ya forodha katika
kuimarisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
aziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya Shirikika la
ndege la Tanzania (ATCL) kupanua huduma zake na kufika Bujumbura nchini
Burundi, ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi
Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja ya hatua za kuimarisha
usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara hiyo Amantius Msole.
…………………………….
Na Frank Mvungi
Serikali
ya Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Nyanja za miundombinu.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mh.Sitta
alibainisha kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 Mawaziri wa Tanzania, Burundi,
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana kujadili namna ya
kuimarisha miundo mbinu ya barabara, reli, anga, anga na maji.
Mh.Sitta
aliongeza kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirikika la ndege
la Tanzania (ATCL) lipanue huduma zake na kufika Bujumbura nchini
Burundi ambapo ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na
Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama hatua za awali za
utekelezaji.
Mh.
Sitta alisisitiza kuwa katika mkutano wa 8 wa Baraza la la Mawaziri la
Jumuiya hiyo umeridhia mfumo wa himaya moja ya Forodha na mpangokazi
unaoainisha masuala ya utekelezaji katika kipindi cha miezi sita ili
kuwezesha kuanzishwa kwa himaya hiyo ifikapo Juni 2014.
Mh.
Sitta akifafanua zaidi alisema mfumo wa himaya moja ya forodha
unaainisha utaratibu wa mzunguko wa biashara, usimamizi wa mapato na
mfumo wa kisheria.
Katika mfumo huo Sitta alisema kuwa ilikubalika kuwa nchi wanachama zitakusanya mapato yake ya kodi.
Aidha,
kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kuelekea nchi nyingine wanachama za
Jumuiya hiyo zimekubaliana kuwa nchi husika itakusanya mapato yake na
kuifahamisha mamlaka ya forodha mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa
kwa ajili ya kuruhusu bidhaa kuondoshwa.
Mkutano
wa 15 wa Kawida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Afrika Mashariki
Uliofanyika Jijini Kampala, Uganda Novemba 30, 2013 na kuamua masula
muhimu ya maendeleo ya Mkutano wa Jumuiya Afrika Mashariki.
Baadhi
ya masuala yaliyojadiliwa na kutolewa uamuzi ni pamoja na kutiwa saini
kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha, kuidhinishwa uundwaji wa Himaya ya Umoja
wa Forodha (Single Customs Territory).
No comments:
Post a Comment