skip to main |
skip to sidebar
WASOMALI KUCHEZESHA YANGA NA WACOMORO
Na Boniface Wambura, Ilala
SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Komorozine
Sports ya Comoro.
Mechi hiyo ya
kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya
Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani
Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi
Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Timu ambazo zimeingia moja kwa moja
katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon,
El Ahly (Misri), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El
Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo
mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na
Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya
Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi
hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed
Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi
hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.Timu
zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni
Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri),
Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy
(Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia)
No comments:
Post a Comment