Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 4, 2014

SHEREHE YA MAOFISA WA JESHI L SHEREHE YA MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA YA KUAGA MWAKA 2013 NA KUUKARIBIS​HA MWAKA MPYA YAFANA JIJINI DAR



mag1 ef374
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) katika sherehe za kuaga Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014. Sherehe hizo zimefanyika jana katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
mag2 4ab98
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza mmoja wa Maofisa wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajin Luckson Mtenga ambaye amezawadiwa zawadi ya Kipoza Joto kutokana na kutenda kazi zake kwa kujituma na kuonesha nidhamu kiutendaji kwa Mwaka uliopita wa 2013.
mag3 60e62
Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakipata vinywaji vya aina mbalimbali katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
mag4 386e8
Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili ya kutosi glasi za vinywaji katika Sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
mag5 c9b29
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Magereza(waliosimama) ambapo wamezawadiwa zawadi ya Kipoza Joto(Refregerator) kila mmoja kutokana na kutenda kazi zao kwa kujituma kwa Mwaka uliopita 2014(wa pili kulia) ni Mke wa Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Frola Minja(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga.

No comments:

Post a Comment