WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
SERIKALI MAKANDANA –TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. DAINA D/O
KIHABA, MIAKA 80, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA SYUKULA ALIFARIKI
DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU ALIJERUHIWA
KWA KUKATWA PANGA KICHWANI NA MIKONONI TAREHE 19.01.2014 MAJIRA YA SAA
21:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SYUKULA, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE
NA HOSEA S/O MWAISWELO, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
SYUKULA. CHANZO KINACHUNGUZWA HATA HIVYO UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA
MTUHUMIWA ANA MATATIZO YA AKILI. MBINU NI KUMVAMIA MAREHEMU AKIWA NDANI
YA NYUMBA ANAKULA CHAKULA NA MJUKUU WAKE ESTER D/O KITWIKA, MIAKA 9,
KYUSA, MWANAFUNZI S/MSINGI SYUKULA STD IV AMBAYE ALIJERUHIWA NA KUPATIWA
MATIBABU KISHA KURUHUSIWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII PALE WANAPOKUWA NA MGONJWA/WAGONJWA WA AKILI NI VIZURI
KUHAKIKISHA ANAPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA TIBA ILI KUEPUSHA MADHARA YA
AINA YOYOTE KWAKE NA KWA JAMII NZIMA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA MOTO.
MNAMO
TAREHE 21.01.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO ENEO LA MWANJELWA, KATA
YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. MFIKEMO S/O OSIA,
MIAKA 50, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA BLOCK Q ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO
KWA VYUMBA VIWILI VYA MADUKA YA NGUO MALI YA WAPANGAJI WAKE WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA VICK D/O ? NA MELELE S/O ? NA
KUSABABISHA MALI YOTE KUTEKETEA. DUKA HILO LINA JUMLA YA VYUMBA VITANO.
CHANZO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA
HAIJAFAHAMIKA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. MOTO HUO
ULIZIMWA NA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA POLISI
NA WANANCHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI
KWA KUCHUKUA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUTOKEA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – AJALI YA UPEPO.
MNAMO
TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA VITONGOJI VYA
MLIMA RELI, CHAPAKAZI NA MTAKUJA VILIVYOPO KATA YA UTENGULE USONGWE,
TARAFA YA BONDE LA SONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.
UPEPO MKALI [KIMBUNGA] ULIOAMBATANA NA MVUA ULISABABISHA ATHARI KUBWA
KWA KUEZUA MAPAA YA NYUMBA 15 ZA KUISHI WATU, VIBANDA VYA BIASHARA 18 NA
KANISA MOJA EAGT. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI
HALISI YA UHARIBIFU BADO KUFAHAMIKA IKIWA NI PAMOJA NA IDADI KAMILI YA
FAMILIA ZILIZOATHIRIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment