Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi
kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya
abiria iliyopangwa kuondoka leo Jumanne Januari 07, 2014 saa 3 usiku
kwenda bara imeahirishwa hadi keshokuwa siku ya Alhamis Januari 09,
2014, saa 3 usiku.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Taarifa
imefafanua kuwa dharura hiyo imetokana na ajali ya treni ya mizigo
iliyotokea juzi saa 2 usiku kati ya Stesheni za Luiche na Kigoma na
kusababisha treni ya abiria kutoka Kigoma kushindwa kuondoka kuja Dar.
Wahandisi
na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio tokea juzi usiku na taarifa
za uhakika zinaeleza kuwa zoezi la kuondoa mabehewa matatu ya treni ya
mizigo yalioanguka na kukarabati njia ya treni litakamilika leo Jumanne
Januari 07, 2014.
Aidha
taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na
kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 07, 2014
No comments:
Post a Comment