Askari polisi akimuongoza mama wa watoto hao polisi |
Askari wanaharakati wa dawati la mtandao wa jinsia kulia na kushoto wakiwa wamemkamata mama wa watoto hao tayari kwenda polisi |
Hapa wakiingia na mama huyo katika ofisi za dawati la jinsia mkoa wa Iringa |
Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Iringa ,Atupele Mwambunda akiwatazama watoto hao nje ya ofisi ya dawati la jinsia mkoa wa Iringa.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Mama wa watoto hao Watende Sanga akiendelea kupika chakula baada ya watoto kuchukuliwa na polisi
Askari wa dawati la jinsia Iringa akiingia kumsimamia mama wa watoto hao kufunga duka lake kabla ya kuchukuliwa kwenda polisi
Mkuu wa
dawati la jinsia mkoa wa Iringa Atupele Mwambunda (kulia) akimhoji
mama wa watoto hao Watende Sanga kuhusiana na ukatili uliofanywa dhidi
ya watoto wake.
....................................................................................................................................................
WAKATI wanaharakati mbali mbali
wakiwemo wanaharakati wa mtandao wa kijinsia Tanzania
(TGNP) ,wanaharakati wa haki za binadam,WAMA kuendelea kukemea na
kuendelea kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia na uyanyasaji
wa wanawake na watoto hata kulifanya jeshi la jeshi
la polisi kuanzisha dawati maalum linaloshughulikia vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia ,baba wa kambo Mussa Mdetela aamua kuwatesa
kinyama watoto wake kwa kuwachoma moto miguu wakituhumiwa kuiba Tsh
10,000
Wakizungumza kwa shida na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com watoto
hao Baraka Rajab Mohamed anayesoma darasa la kwanza na Mood Rajab
Mohamed anayesoma darasa la sita walisema kuwa ilikuwa ni siku ya
tarehe 3 ambapo walichukua pesa hiyo kiasi cha Tsh 10,000 na kwenda
kununua chakula baada ya mama yao kushindwa kuwaandalia chakula.
Hata hivyo
Mood anayesoma darasa la sita msingi Lugalo alisema kuwa siku
ya tukio mdogo wake alikwenda ndani na kuchukua kiasi hicho cha
fedha na baada ya muda walishirikiana katika matumizi .
Watoto hao
ambao wanadai kuwa baba yao mzazi Rajab Mohamed aliwaacha na sasa
anaishi jijini Dar es Salaam na wao wamekuwa wakiishi na baba yao
mdogo huyo ambae mara kwa mara amekuwa akiwaadhibu vikali.
Kwani walisema kuwa
kutokana na mara kwa mara kushinda bila kula ndipo siku hiyo
walipoamua kuchukua pesa hiyo ili kununua bagia na vitumbua ili
kujikimu kwa njaa .
Hata hivyo walisema
baada ya baba yao kurudi kutoka katika shughuli zake na kubaini
kuwa fedha hiyo imechukuliwa ndipo alipowakamata na kuwafunga kamba na
kuanza kuwatesa kwa kichapo ili waweze kusema mtu aliyechukua
pesa hiyo.
“Alitufunga
kamba miguuni na mikononi na kuanza kututesa kwa kutupiga na baada ya
kuona hatusemi ndipo alipochukua makaratasi ya naironi na kutufunga
miguuni kisha kuchukua kiberiti ,mafuta ya taa na kuwasha moto katika
miguu yetu huku akiendelea kutupiga na moto ukiwaka miguuni….wakati huo
mama alikuwa amekaa mlangoni akishangilia kuwa wapige sana
mimi nimewachoka hawa watoto heri wafe tu” walisema watoto hao
Atupele Mwambunda mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Iringa ameuthibitishia mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com juu ya tukio hilo na kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na kamwe hakitavumilika.
Alisema
kuwa kuanzishwa kwa dawati hilo ni kutaka kukomesha vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia kama hivyo na kuwataka wazazi na jamii kuepuka
kuchukua sheria mkononi kwa kuwatesa watoto kama hao ambao
mwisho wa siku wanapoteza mwelekeo wa maisha.
Mwambunda alisema kuwa
hadi sasa wamefanikiwa kumkamata mama wa watoto hao Watende Sanga
huku mzazi mwenzake Mussa Mdetele bado anatafutwa na jeshi la polisi
ili kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatesa watoto hao.
Huku
mama wa watoto hao akidai kuwa wakati baba yao mdogo akiwapiga watoto
hao yeye hakujua kinachotokea japo alikuwa na taarifa ya kupotea
kwa pesa katika duka na kuwa baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa ili
kuwatibu kinyemela pamoja na kuwaombea ruhusa shuleni .
No comments:
Post a Comment