Kijana
Felix, mkazi wa Mbalizi akiwa katika hospitali teule ya wilaya ya
Mbeya,(Ifisi-Mbalizi), akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na mabati
kichwani yaliyotokana na kimbunga.
|
Katibu
tarafa wa tarafa ya Songwe, Felix Lyaniva, akijionea uharibifu wa
baadhi ya nyumba za wanancho eneo la Mtakuja Mbalizi, baada ya kuezuliwa
na kimbunga.
|
WATU zaidi ya
saba wamejeruhiwa na mapaa ya mabati yaliyoezuliwa na kimbunga
kilichotokea eneo la Mbalizi majira ya saa saba mchana, wilaya ya Mbeya
Vijijini mkoani hapa.
Kikosi kzi cha kalulunga media, kilifika eneo la tukio na kujionea
hali halisi n kukuta baadhi ya familia zikiwa zimekosa makazi ya kuishi
baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na baadhi ya vitu kutoonekana katia
makzi yao.
Maeneo ambayo yameathirika zaidi ni pamoja na eneo la Mtakuja,
Chapakazi na Tarafani ambako maduka zaidi ya nane yaliezuliwa na bidhaa
kupotea huku vibaka na wakijitwalia mali hizo kwa kupigana kabla na
baada ya kufika askari.
Wakati wa tukio hilo, umeme ulileta hitilafu katika kamazi mengi
kutokana na upepo mkali kung'oa nyaya katika makazi ya wananchi ambapo
watumishi wa Tanesco walifika eneo la tukio na wanatarajia kuanza
kufunga umeme huo kesho kwa mujibu wa maafisa wa tanesco waliofika eneo
la Tukio.
Muuguzi mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Mbeya, Dr. Sikitu
Mbilinyi, alithibitisha kupokea baadhi ya majeruhi katika hospitali hiyo
na kuwaruhusu baada ya kuwapatia matibabu.
Wakati huo huo, ajali ya Lori aina ya Volvo, limegonga magari zaidi
ya matano eneo la stendi ya Zamani Mbalizi lakini hakuna vifo
vlivyotokea katika matukio yote mawili.
CHANZO kalulungablog
No comments:
Post a Comment