Mume
wa marehemu Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye
harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa
wetu marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2
usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika harambee iliyofanyika
Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi kilichokuwa
kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya kweli
shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine
lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa
kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera.
WanaDMV tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii
kuja kusaidia kutimiza malengo.
Shangazi
wa marehemu Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera
huku akiwa amejawa na uso wa huzuni aliwashukuru wote waliofika kwani
lengo ni kusaidia kuchangia ili mwili wa marehemu Zainab uweze
kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na matarajio ni kusafirisha
siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne jioni
mahali patatangazwa baadae.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa harambee.
Dada Tuma akielezea utaratibu wa mnada utakavyokuwa.
Washika mahesabu wakijiweka sawa kabla ya harambee kuanza.
Watanzania waliofiika kwenye harambee wakitoa michango yao kabla ya harambee haijaanza
Michango ikiendelea kabla ya harambee.
Timu ya New York ikitoa mchango wake.
Dada Tuma akiendesha mnada.
Umati wa Watanzania waliokuja kwenye harambee.
Watanzania kutoka New York katika picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni Yunus, Bob Miano, Mmiliki wa Vizion One Abdallah Kitwara na Albert Mateso wakiwa kwenye harambee.
No comments:
Post a Comment