Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akipokelewa Wizarani na Katibu Mkuu Bw. Job Masima. Mhe.
Mwinyi akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel
Ndomba mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani. Kulia kwa Mnadhimu Mkuu ni
Naibu Katibu Mkuu Bibi Mwitango Rose Shelukindo. Waziri Mwinyi akisalimiana na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo Wizarani.TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Mhe.
Nahodha akisaini Hati ya kukabidhi Wizara ya Ulinzi na JKT kwa Waziri
Mwinyi. Kutoka kulia waliosimama wakishuhudia ni Mnadhimu Mkuu wa JWTZ
Luteni Jenerali Ndomba, Katibu Mkuu Bw. Masima na Mkuu wa JKT Meja
Jenerali Muhuga. Mhe. Nahodha akikabidhi rasmi shughuli za Waziri wa Ulinzi na JKT kwa Mhe. Mwinyi. Waziri
wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (wa tatu kutoka kulia) akiwa
na watendaji wakuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT na Taasisi zake mara baada
ya kukabidhiwa shughuli za Wizara hiyo.
…………………………………………………………………….
Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Bw. Job Masima leo amewaongoza wakuu wa
Idara, Vitengo na Taasisi za wizara hiyo kumpokea Waziri wa Ulinzi Dkt
Hussein Mwinyi (Mb) ambaye ameripoti wizarani hapo rasmi baada ya
kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kushika wadhifa huo
hivi karibuni.
Akimkabidhi
wizara hiyo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Shamshi Vuai
Nahodha amemuasa Waziri Mwinyi kuwa pamoja na majukumu yake ni vema
akatenga
muda wa kutembelea miradi ya wizara hiyo, ikiwemo ujenzi wa nyumba ili
kuona mambo yanavyokwenda na kurekebisha dosari kabla miradi haijafika
mbali.
Kwa
upande wake, Waziri Mwinyi amewataka viongozi wa Wizara hiyo kufanya
kazi kwa kasi kubwa kwani kipindi kilichobaki ni kifupi sana kuelekea
kwenye Uchaguzi mkuu ujao.
“Mwaka
uliobaki wa kufanya kazi ni mmoja tu kwani mwaka 2015 utakuwa na mambo
mengi yanayohusiana na uchaguzi hivyo tulenge kufanya kazi kubwa kufikia
malengo yetu ndani ya mwaka huu mmoja kwa kasi kubwa”, alisisitiza Mhe.
Mwinyi.
Aidha,
Mhe. Mwinyi alimshukuru Mhe. Nahodha kwa mambo muhimu aliyoshauri
ikiwepo kukamilisha yale yote aliyokuwa ameyaanzisha kwa maslahi ya
Wizara na Taasisi zake. Alimtakia kila la heri katika majukumu yake ya
uwakilishi na ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla
ya makabidhiano hayo Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi walijipanga kwa
safu ndefu kumpokea Waziri wa Ulinzi na JKT wakiongozwa na viongozi
mbali mbali waliohudhuria makabidhiano hayo wakiwemo Naibu Katibu Mkuu
Bibi Mwitango Rose Shelukindo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali
Samuel Ndomba (aliyemuwakilisha Mkuu wa Majeshi), Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Mzinga Meja Jenerali Charles Muzanila na Wakuu wa Idara na Vitengo wa
Wizara ya Ulinzi na JKT.
Hii
ni mara ya tatu kwa Mhe. Mwinyi kuteuliwa kuongoza Wizara hiyo. Kwa
mara ya kwanza aliteuliwa mwaka 2008 hadi bunge lilipovunjwa wakati wa
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Aidha, aliteuwa tena katika Baraza jipya
mwaka 2010 hadi 2012 alipohamishiwa Wizara ya Afya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ulinzi na JKT
No comments:
Post a Comment