
Na Ali Issa –Zanzibar 31/12/2013
Waziri
wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazurui amesema nyezo muhimu
ya kuendeleza Biashara ni kuanzisha na kuendeleza Tamasha la Biashara
kwa ajili ya mauzo ya Bidhaa mbalimbali zinazo zalishwa viwandani,
bidhaa za wajasairiamali, bidhaa za kilimo na huduma za biashara.
Hayo
ameyasema leo huko Chuo cha Maendeleo na Utalii Maruhubi Zanzibar
wakati alipokuwa na mazungumzo na wandishi wa Habari kuhusiana na
Tamasha la Biashara la miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema
nchi nyingi duniani zimeanzisha matamasha ya biashara kwa lengo la
kuhamasisha na kuendeleza biashara katika nchi zao na kupelekea kuinua
uchumi wa nchi zao.
Amesema
Zanzibar hivi sasa imeona ni vyema na wao kuwa na utaratibu kama huo
kila mwaka ili kuona nayo inapiga hatua kubwa kibiashara na kuimarisha
uchumi wake.
“Nchi
kama Dubai,Singapore, China na nchi nyengine nyingi duniani wanayo
matamasha ya biashara katika nchi zao na imekuwa ni kichocheo kikubwa
cha kukuza biashara,” alisema Mazurui.
Aidha
alifahamisha kuwa lengo kuu la Tamasha hilo ni kuitangaza Zanibar kama
ni kituo maarufu cha Biashara na kuhamasisha biashara, kuendeleza masoko
ya bidhaa na kuitangaza Zanzibar kiutalii.
Alilitaja
Lengo jengine kuwa ni kupatikana Bidhaa kwa bei rahisi, kupata mahitaji
ya bidhaa tafauti katika sehemu moja, kuwaezesha wafanya biashara,
wazalishaji wakuu wa bidhaa za viwandani kukutana na wateja moja kwa
moja na wazalishaji na wafanya biashara kujitangaza kibiashara.
Waziri
Mazrui alisema kua tamasha hilo litaaza tarehe 6 hadi 12 January
2014 katika viwanja vya Maisara ambapo hadi sasa wafanya biashara na
kampuni 100 kutoka ndani na nje ya Zanibar ikiwemo Tanzania Bara,
Uturuki, Syria, Indonesia na nchi nyenginezo zimejitokeza kushiriki
Tamasha hilo.
“Tunawahakikishia
wananchi kwamba bidhaa zitakazoletwa katika Tamasha hili zitakuwa zenye
viwango vya hali ya juu na tutakuwa makini kuona bidhaa feki hazipati
nafasi,” alisitiza Mazrui.
Alisema
tamasha hilo litagharimu shilingi milioni 140 na kila mshiriki wa
kigeni atatozwa dola 300, wandani shilingi 200.000 na wajasiriamali
watatozwa shilingi 100,000 lakini wataruhusiwa kushirikiana zaidi ya
wajasiriamali wawili katika sehemu moja.
Waziri
wa Biashara Viwanda na Masoko aliwataka wafanyabiashara wa Zanzibar
washiriki kwa wingi katika Tamasha hilo wakiwa na bidhaa zenye ubora na
wananchi wajitokeze kununua bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
No comments:
Post a Comment