Mtoto Ismail Barihegi.
MTOTO Ismail Barihegi, mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Fukayosi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ameokotwa akiwa amekatwa mapanga baada ya kudaiwa kuipeleka mifugo yao katika mashamba.
Barihegi
ambaye amelazwa katika Jengo la Mwaisela Wodi na 17, Muhimbili,
alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba siku ya tukio
(hakumbuki)alikuwa akichunga ng’ombe porini lakini ghafla walitokea
watu na kumwuliza kwa nini aliwaachia ng’ombe wake kufika
shambani. Alisema aliwakatalia watu hao kwamba mifugo iliyokuwa shambani
haikuwa ya kwao, na hata kuwaonesha ng’ombe wao, lakini watu hao
hawakumwelewa.
“Walianza kunikata mapanga kichwani, begani na sehemu zingine za mwili, nililia sana huku nikiwaomba wanisamehe hawakunisikia.
“Wenye ng’ombe walishakimbia, waliniambia
ni lazima waniue, niliwaomba wasiniue, lakini hawakunijali, niliishiwa
nguvu, damu nyingi ilikuwa imenitoka,waliondoka na kuniacha porini peke
yangu.
“Nilipiga kelele ili nipate msaada lakini
hakuna aliyejitokeza, nilikata tamaa, baada ya saa kadhaa mtu mmoja
alipita na kuniona, akawaita watu akiwemo Mwenyekiti wa kijiji chetu,
wakaja kunichukua na kunikimbiza katika zahanati,” alisema mtoto huyo.
Kijana huyo alisema kwamba baada ya huduma
ya kwanza katika zahanati hiyo, alihamishiwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili baada ya hali yake kuonekana mbaya zaidi na kwamba ana uhakika
wazazi wake hawajui alipo kwani hadi sasa hawajafika kumtembelea.
“Ninamshukuru sana mwenyekiti kwa kunipa
msaada mkubwa, sasa hivi amerudi kijijini, najua atawapa taarifa ndugu
zangu, ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa kuokoa maisha yangu kwani
kwa sasa nina nafuu tofauti na nilivyookotwa katika msitu mnene,”
alisema Barihegi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani, Athumani mtasha alipoulizwa kuhusiana na tukio alisema kuwa amehamishiwa makao makuu.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, SACP Urich
matei yupo nje ya mkoa kikazi ila kaahidi kufuatilia sakata hilo kwa
undani.NA GLOBAL PUBLISHER
No comments:
Post a Comment