Mbunge
wa Temeke Abbas Mtemvu akimkaribisha Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum, alipowasili kwenye ukumbi, baada ya kuwalikwa
kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo hilo, ambao uliambatana na uchaguzi wa
Mwenyekiti wa Jimbo na Katibu ambapo katika jumla ya kura 54
zilizopigwa Ahmad Mnamala alipata kura 50 za ndiyo na tatu za hapana na
hivyo kuibuka mshindi, huku kwa jumla ya kura hizo hizo zilizopigwa,
Kasim Kiame akiibuka kuwa Katibu wa jimbo kwa kupata kura zote 54 za
ndiyo.
Sjeikh Salum akisalimiana na Mtangazaji wa Channel Ten, David Ramadhan
Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,
akisalmiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke, Sikunjema Shabani,
baada ya kuwasili ukumbini.
Mtemvu, Sheikh Salum na Mwenyekiti wa CCM wilaya wakishangilia kabla ya kukaa vitini kuruhusu kikao kuanza
Wajumbe nao wakiwa wamesimama kuwalaki viongozi wa meza kuu
Meza ya ufundi ikiwa kazini kuhakikisha itifaki zote zinakwenda sawa
Sheikh Salum akizungumza mwanzoni mwa
mkutano huo ambapo alisisitiza msimamo wake kuwa yeye ni Muumin wa
serikali mbili na kuwataka wajumbe wa mkutano huo nao kuamini hivyo. Pia
aliwatakia uchaguzi mzuri wakimtanguliza Mungu mbele ili kumpata
kiongozi atakayelisaidia jimbo hilo la Temeke
Sheikh Salum akishikana mkono na Mtemvu baada ya kuzungumza
Mwenyekiti wa CCM wilaya aya Temeke akizungumza
Ahmad Mnamala akiomba kura kwa wajumbe wakati akijieleza
Kasim Kiame akiomba kura za kuwa katibu wa jimbo
Wajumbe wakigawiwa karatasi za kura
Baadhi ya wajumbe wakipiga kura.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment