RPC Mungi
Mwandishi Diana Bisangao wa matukiodaima.com
.............................
Watu
wawili wafariki dunia katika matukio manne tofauti mkoani Iringa
likiwemo la mzee wa miaka 90 kujinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge
nyumbani kwake.
Akizungumza ofisini
kwake Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Iringa Nyigesa Wankyo alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 16 februari majira ya
saa 11:04 jioni.
Kaimu kamanda Wankyo alimtaja mzee huyo aliyejulikana kwa jina Dauson Mlonganile mkazi wa kijiji cha Nundwe wilayani Mufindi.
Wankyo alisema chanzo cha tukio hilo ni kuugua kwa muda mrefu kwa mzee huyo.
Katika tukio lingine mtu mmoja mwanaume alikutwa ndani ya shamba la mpunga akiwa amefariki dunia.
Kaimu
Wankyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 14
februari majira ya saa 2 kamili usiku katika kijiji cha Makifu wilaya
ya Iringa vijijini.
Hata
hivyo alisema marehemu huyo alikufa kutokana na ugonjwa wa kifafa
kumpanda wakati akiendelea na shughuli zake za kilimo zikiwemo za
kupanda mpunga, mwili wa marehemu umezikwa na ndugu zake.
Wakati
huohuo JESHI la polisi mkoani Iringa linamtafuta mtuhumiwa
aliyejulikana kwa jina moja la Cley kwa kosa la kumbaka mwanafunzi jina
limehifadhiwa(19) mkazi wa Kihesa na kumsababishia maumivu makali sehemu
za siri.
Kaimu
Wankyo alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 februari majira saa
9 kamili mchana na kusema mtuhumiwa huyo alimkaribisha mwanafunzi
chumbani kwake na kumvua nguo kisha kumbaka.
Chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya mwili na mtuhumiwa bado anatafutwa.
Mbali
na matukio hayo matatu, Kaimu Wankyo alisema JESHI la polisi
linamshikilia Elisante Benya (27) mkazi wa Frelimo kwa kosa la kukutwa
na madawa ya kulevya aina ya bhangi.
Kaimu
Wankyo alithibitisha tukio hilo lililotokea tarehe 16 februari majira
ya saa 8 kamili mchana maeneo ya kuuzia pombe za kienyeji barabara mbili
kata ya makorongoni ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na kete 5 pamoja na
msokoto mmoja akiwa ameyahifadhi ndani ya mfuko wa koti alilokuwa
amelivaa.
No comments:
Post a Comment