Boniface
Mkwasa kocha msaidizi wa Young Africans mchana huu anaondoka kuelekea
jijini Cairo nchini Misri kwenda kushuhudia mchezo wa Fainali ya (Super
Cup) Mshindi wa Klabu Bingwa Afrika timu ya Al Ahly ya Misri dhidi ya
Mabingwa wa Kombe la Washindi Afrika timu ya CS Sfaxien ya Tunisia
mchezo utakaofanyika siku ya Alhamis katika dimba la Cairo International
Stadium.
Mkwasa
anandoka kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia Airline ambapo
atapitia jijini Adis Ababa kabla ya kuunganisha kuelekea Cairo ambapo
atatua Uwanja wa Ndege majira ya saa 7 usiku na kupokelewa na wenyeji
kutoka ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Misri.
Kutokana na umuhimu wa mchezo huo
Uongozi wa Young Africans kwa
pamoja na Benchi la Ufundi walikaa na kukubaliana kuwa kocha msaidizi
Mkwasa aende kushuhudia mchezo huo wa fainali ambao utaweza kusaidia
kupata picha ya wapinzani Al Ahly ambao watacheza na Young Africans
mwishoni mwa mwezi huu.
Lengo la
safari ni kuweza kuwaona Al Ahly wanavyocheza katika mchezo huo wa
fainali, pili ni kujua wanayocheza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani
na tatu ni kuijua timu nzima kiufundi inachezaje.
Kwa
upande wake Kocha Mkwasa amesema anaamini ataitumia vizuri nafasi hiyo
ya kuutazama mchezo wa Super Cup kwa kuwasoma wapinzani na pindi
atakaporejea atasaidiana na kocha mkuu kuwaandaa vijana tayari kwa
mchezo huo.
Mkwasa
mara baada ya kuutazama mchezo huo dhidi ya CS SFaxien siku ya Alhamis
jioni saa 11 kamili kwa saa za Afrika Mashariki atarejea nchini siku ya
ijumaa n akuungana na kikosi kwa ajili ya mchezo wa siku ya jumamosi
dhidi ya timu ya Ruvu Shooting.
Al
Ahly Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa Barani Afrika watacheza na Young
Africans Tarehe 1 Machi 2014 katika mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia
katika 16 bora kisha kurudiana jijini Cairo wiki moja baadae
No comments:
Post a Comment