Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani
Dodoma David Misime amesema chanzo cha kifo cha Mtoto huyo mwenye umri
wa
miaka miwili ni ubovu wa nyumba na ukuta uliokuwa umeloana kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha jambo lililopelekea kuanguka na kusababisha
kifo hicho.
Aidha Kamanda Misime amesema ukuta huo uliwaangukia Bi Hadija
Mtoro mwenye umri wa miaka 80 na Marehemu wakiwa wanapika chakula cha
jioni majira ya saa moja na dk 50 ambapo baada ya kuangukiwa mama huyo
alipiga kelele kuomba msaada ndipo majirani wakafika eneo La tukio na
kutoa msaada huo.
Baada ya majirani kuondoa matofali yaliyokuwa juu yao
waliwabeba majeruhi na kuwapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
ndipo ikabainika
kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa uchunguzi wa daktari.Na Dodoma Fm
No comments:
Post a Comment