Wakizungumza na Dodoma fm wakazi hao wamesema wamekuwa
wakitoa michango ya ulinzi lakini hakuna utendaji kazi wowote
unaofanyika.Naye bwana Amasha Shaban mkazi wa mtaa huo ameitaka kamati
ya ulinzi shirikishi kuweka ulinzi wa kutosha mtaani
hapo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ulinzi shirikishi amekiri kuwepo
kwa michango hiyo ambayo huwasaidia katika matumizi mbalimbali ikiwemo
kununua vifaa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.Sanjari na hayo mwenyekiti
ameeleza kuwa kuna changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo
ujuzi mdogo katika suala la ulinzi.
Viongozi wa kijiji cha solowu wilayani chamwino Mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuwapelekea
chakula cha msaada kutokana na njaa kukithiri kijijini hapo.
Akizungumza na kituo hiki mwenyekiti wa kijiji cha Solowu bw. Omari Salimu amesema hali ya njaa kijijini hapo
ni kubwa hivyo inawafanya wakulima wengi washindwe kulima mashamba yao katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea
kunyesha.
Nae afisa Maendeleo wa kijiji hicho Bw Yohana Messai ameitaka
serikali kupeleka chakula cha bei rahisi ili kunusuru wimbi la
njaa kijijini hapo.Kwa upende wake mkuu wa wilaya ya Chamwino Bi
Fatma Ally amekiri kuwepo kwa upungu wa chakula
katika baadhi ya vijiji na hivyo amewataka wakulama kulima mazao
yanayostahimili ukame.Na Dodoma Fm
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment