Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, February 5, 2014

Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,Mahmoud Thabit Kombo aapishwa rasmi Zanzibar.

Mhe Mhmoud Thaib Kombo, akiapishwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi kuwa Mwakilishi wa Jimbola Kiembesamaki, baada ya kushinda Jimbo hilo na kuwa Mwakilishi Mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.    
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kuapishwa kwa Mhe. Mahmoud Thaib Kombo, baada ya kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo la kiembesamaki Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM. 
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar kwa kupata ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika wiki iliopita.
Mhe. Spika wa Baraza la Mapinduzi Pandu Ameir Kificho akimkabidhi Vitendea Kazi vya Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.




Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akifurahi baada ya kuapishwa akiwa na Mwakilishi wa Bububu Mhe.Husein
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja na familia yake na Waheshimiwa wa Baraza nje ya Ukumbin wa Baraza la Wawakilishi baada ya kuapishwa.



Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakimshangilia Mwakilishi wao nje ya Majengo la Baraza la Wawakilishi.
Mhe. Mahmoud Thabi Kombo akiwashukuru wananchi wa jimbo la kiembesamaki kwa mashirikiano yao tangu mwazo wa kampeni hadi kupiga kura na kumchagua kuwa mwakilishi wao. 

No comments:

Post a Comment